Rafiki leo tunaendelea na kanuni zitakazotutoa chini kwenda juu katika mfumo wetu wa kimaisha na kibiashara, leo nakukaribisha tujifunze kanuni ya kuamini. Rafiki imani ni jambo muhimu katika kukamilisha mambo huyatakayo, ukisoma biblia inasema " hata kama una imani ndogo kama punje ya haladai, ukiamuru mlima ung'oke na ukajitose baharini nao utang'oka", hapa tunaona imani ina nguvu sana katika maisha yetu, ukiamini huwezi na hutaweza kweli, na ukiamini kuwa unaweza kufanikiwa na utafanikiwa hivo chochote unachokiamini kweli kinakuja kuwa uhalisia.
siku zote unatenda kile unachokiamini hasa unavyojiamini mwenyewe, hivyo kama wewe mwenyewe unaamini kuwa wewe ni dhaifu huwezi fanya mambo makubwa, huwezi kuamini kile unachokiona ila unaona kitu ambacho tayari unakiamini. jambo la msingi rafiki kataa taarifa zozote ambazo zitakuchanganya kwa kile unachokiamini, mfano watu walioshindwa wanapenda kuwaaminisha wengine kwamba hawawezi kufanya jambo walilolishindwa wenyewe. Soma Hakuna kinachoshindikana kama ukiamua.
Rafiki gharama ya kuamini ni kujiwekea mipaka katika kuamini (self limiting beliefs), hii inatokea pale ambapo unapoanza kujiwekea mipaka katika mambo mengine. Mfano, unapoamini wewe una kipaji kidogo au huna kipaji kuliko wengine, unapoamini kwamba mwingine anaweza kuliko wewe, hapo utakuwa umejiwekea mipaka juu ya kile unachokiamini na siku zote utakuwa kama vile unavyoamini.
Mipaka inakuwa ni kizuizi katika mafanikio uyatakayo, inakurudisha nyuma na kuzaa maadui wawili katika maisha yako ambao ni Hofu na Mashaka, ambao wanakufanya kila siku ubaki palepale. Rafiki kataa udhaifu huu na acha kujiwekea mipaka katika kuamini, amini unaweza kufanikiwa kama ukiweka juhudi na ufanisi kwa kile ukifanyacho. Soma Tumia hasira yako kuchukia udhaifu wako
Mpendwa rafiki sheria hii inasema amini hakuna mtu bora kuliko wewe na hakuna anaeweza zaidi yako, anza sasa kuachilia kile unachopenda kukifanya na kifanye kwa ufanisi mkubwa na amini kwamba utafanikiwa.
Rafiki mimi nikutakie siku njema na yenye mafanikio makubwa, acha hofu na mashaka katika maisha yako, acha kujiwekea mipaka amini unaweza kufanya jambo na ukafanikiwa. Siku zote amini wewe ni bora kuliko wengine na una uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba