Soko ni sehemu ambayo watu wanakutana kwa ajili ya kuuza au kununua bidhaa ama huduma fulani. Kabla ya kuanza biashara, mjasiriamali anashauriwa kufahamu kuhusu masoko na kama bidhaa/huduma anayotaka kuuza itauzika au hapana, na kulifanya hili mjasiriamali anatakiwa kufanya utafiti wa masoko. Na kwa bahati mbaya, wajasiriamali wadogo wengi huwa hawafanyi utafiti wa masoko hadi mshindani wa kibiashara afungue biashara karibu na ya kwake. Katika suala la masoko, mjasiriamali anashauriwa kuwajua mapema washindani wake kibiashara ili aweze kutengeneza mipango ya kuumudu ushindani uliopo.
Kufanya utafiti juu ya washindani wako wakibiashara itakusaidia kufahamu udhaifu na uimara wao kibiashara. Kwa kufahamu masuala haya utakuwa katika wakati mzuri wa kupangilia biashara yako kwa kufahamu ni aina gani ya bidhaa unazotakiwa kutoa, ubora unaopendelewa na wateja, na namna ya kuiweka biashara yako kitofauti. Hatua zifuatazo zitakusaidia namna ya kumfahamu mshindani wako kibiashara:
Hatua ya I: Watambue washindani wako
Kila biashara inakuwa na mshindani na unahitaji kuchukua muda kujua sehemu nyingine ambayo wateja wako wanaweza kupata huduma au bidhaa kama unazouza. Hata kama bidhaa zako ni za kibunifu sana, unashauriwa kuangalia bidhaa nyingine ambazo ni mbadala wa bidhaa zako ambazo zinaweza kuleta ushindani.
Anza kwa kuangalia washindani wako walio karibu na eneo la biashara yako. Hapa unapaswa kuangalia biashara zinazofanya vizuri sokoni kwa wakati huo, kwa mfano, kama wewe ni muuza matunda angalia muuza matunda wa karibu yako na kadhalika.
Halafu angalia washindani wako wengine ambao siyo wa moja kwa moja. Hawa ni washindani ambao hakuna ushindani wa moja kwa moja lakini wanalenga soko kama la kwako kwa ujumla, kwa mfano, mtemebezaji wa matunda ambaye huwa anapitisha maeneo biashara yako ilipo.
Mwisho kabisa angalia washindani wanaoweza kuja kwenye maeneo karibu na biashara yako ili kuleta ushindani mpya.Kwa hiyo, ni lazima ujiandae hata kwa ushindani ambao haupo ila unadhani unaweza kuwepo siku zijazo.
Anza kwa kuangalia washindani wako walio karibu na eneo la biashara yako. Hapa unapaswa kuangalia biashara zinazofanya vizuri sokoni kwa wakati huo, kwa mfano, kama wewe ni muuza matunda angalia muuza matunda wa karibu yako na kadhalika.
Halafu angalia washindani wako wengine ambao siyo wa moja kwa moja. Hawa ni washindani ambao hakuna ushindani wa moja kwa moja lakini wanalenga soko kama la kwako kwa ujumla, kwa mfano, mtemebezaji wa matunda ambaye huwa anapitisha maeneo biashara yako ilipo.
Mwisho kabisa angalia washindani wanaoweza kuja kwenye maeneo karibu na biashara yako ili kuleta ushindani mpya.Kwa hiyo, ni lazima ujiandae hata kwa ushindani ambao haupo ila unadhani unaweza kuwepo siku zijazo.
Hatua ya II: fahamu udhaifu wao
Baada ya kuwafahamu washindani wako kibiashara, fahamu udhaifu wao ni nini kibiashara. Kwa nini wateja hununua bidhaa kutoka kwako? Je, ni kwa sababu ya bei? Ubora wa bidhaa? Huduma? Au ni kwa sababu ya sifa nzuri aliyojijengea kwa wateja? Jitahidi kuweka malengo juu ya kufahamu mambo haya.Hii ni kwa sababu mtazamo wa wateja juu ya bidhaa yako ni muhimu sana.
Ni vizuri zaidi kufanya uchunguzi huu wa uimara na udhaifu wa mshindani wako kwa kutumia jedwali. Andika jina la kila mshindani wako na sifa alizokuwa nazo. Ni muhimu kufahamu masuala ya msingi kama vile bei, ubora, muonekano wa bidhaa, eneo la biashara, njia za mauzo nakadhalika. Baada ya kuandaa jedwali hilo, anza kuwaweka kwa namba juu ya upinzani wanaokupa kibiashara kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho na sababu za kuwaweka kwenye namba tofauti kulingana na ushindani wao kwako.
Hatua ya 3: Angalia fursa na Vitishio vya kibiashara.
Fursa na vitishio vya kibishara ni miongoni mwa masuala yaliyo ndani ya udhibiti wa kampuni.Pindi unapomunagalia mshindani wako kibiashara pia unatakiwa kufahamu ni kwa namna gani amejipanga kutatua mambo yaliyo nje ya uwezo wake.Masuala haya huitwa fursa na vitisho vya kibiashara.
Fursa na vitisho vy kibiashara ni vya namna mbali mbali.Vinaweza kuwa upande wa teknolojia, masuala ya kikanuni au kisheria, masuala ya kiuchumi au hata mshindani mpya. Kwa mfano, mfanyabiashara ya kupiga picha anapaswa kufahamu ni kwa kiasi gani wapiga picha wengine wamejiandaa kuendana na teknolojia ya digitali ya upigaji picha.
Njia nzuri ya kufahamu fursa na vitisho vya kibiashara ni kupitia jedwali litakalokuwa na majina ya washindani wako na kuweka na masuala yanayoweza kuathiri biashara yako.Baada ya hapo sasa unaweza kufahamu namna unavyoweza kushughulikia fursa na vitisho vya kibiashara.
Hatua ya 4: Amua nafasi yako
Baada ya kufahamu udhaifu na uimara wa washindani wako kibiashara na fursa na vitisho kwenye biashara, unatakiwa kuamua wewe una nafasi gani katika ushindani wa kibishara na washindani wako kwa kuzingatia namna biashara yako inakwenda. Hii itakupa picha nzima juu ya wapi ilipo biahsara yako kulingana na washindani wako katika eneo mlipo. Pia itakusaidia kufahamu maeneo ya biashara yako ambayo unatakiwa kuyaboresha na sifa gani ya biashara yako unayotakiwa kuitumia kukuletea wateja zaidi ili upate wateja zaidi.
Ili ufanikiwe katika biashara yako ni lazima ufanye utafiti wa soko la biashara yako hii itakufanya ujue ni huduma gani ambayo wateja wanahitaji na wewe kuanza kutoa huduma.