SHERIA 3: MVUTO (LAW OF ATTRACTION)

Habari za muda huu mpendwa rafiki, nakukaribisha kwa Mala nyingine katika kujifunza sheria na kanuni mbalimbali zitakazotuongoza katika kupata mafanikio katika maisha yetu na biashara zero. Leo tutaenda kuiangalia sheria ya mvuto(the law of attraction), rafiki duniani tunaishi kama sumaku inabidi uvutie katika maisha yako na ya watu wengine. Karibu tujifunze kwa pamoja kanuni hii.
Sheria ya mvuto(law of attraction) hii ni moja ya sheria kubwa zinazoelezea sana kuhusu kufanikiwa na kutokufanikiwa katika biashara na maisha binafsi. Sheria hii iliandikwa na imezungumziwa miaka 3000 kabla ya kristo, ni sheria yenye nguvu sana inayogusa kila kitu unachofanya au unachosema au unachofikiri au kuhisi.
Kila kitu ulichonacho katika maisha yako, unajivutia mwenyewe kwa namna unavyofikiri, kwa sababu ya vile ulivyo. Rafiki utaweza kubadili maisha yako kama utaweza kubadili namna ya unavyofikiri. 
Kuna msemo unaosema "ndege wafananao ndio huruka pamoja", "kizuri huvutia kizuri", "chochote unachokitaka nacho kinakutaka" misemo hii ni njia ya kuelezea sheria ya mvuto (law of attraction).
Kampuni zinazalisha bidhaa na kutoa huduma na namna ya kufanya biashara kwa namna itakavyowavutia wateja,wafanyakazi, wasambazaji, na mzunguko mzima unaounganisha kampuni. Kitu chochote kisipoenda vizuri katika kampuni,  haraka marekebisho yanafanyika ili kurudisha mahusiano mazuri katika kampuni,  rafiki naamini ushawahi kusikia mfano tanesco wakitaka kukata umeme kwa ajiri ya matengenezo wanasema tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. 
Nguvu ya mvuto inategemea sana lugha nzuri, mahusiano mazuri kati ya wewe na mteja wako, lugha nzuri itamvuta mteja aje kwenye biashara yako muda mwingine,  hapa ndipo unaona kwanini biashara za watu wengine zinaharibika hii ni kwasababu watu wengi wameshindwa kuwavutia wateja kuja tena na kufanya kila siku biashara irudi nyuma zaidi kuliko kusonga mbele.
NAMNA YA KUITUMIA SHERIA YA MVUTO
-Toa huduma bora kwa wateja wako.
-Lugha nzuri itawale katika biashara yako.
-kipe thamani kila kitu unachokifanya kwa sababu utawavutia watu kwa ile thamani uliyoitoa kwa biashara yako.
-Jiulize mwenyewe kipi kinakufanya usifanikiwe katika biashara yako kisha fikiria ni mabadiliko gani unayoyahitaji,  kama unahitaji mabadiliko, badilika wewe Kwanzaa. 
Nikitakie siku njema mpendwa rafiki fanyia kazi sheria hii naamini hutabaki kama ulivyokuwa. Tukutane katika sheria nyingine katika kujifunza zaidi.
          " Your choice, your life"