Sifa kubwa ya binadamu ni kukua kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, ili kufikia mafanikio makubwa mi lazima ukubali kubadilika na kukua. Leo napenda nikushirikishe sababu tisa zinazomfanya mtu kukua na kufikia mafanikio makubwa, sababu hizi ni lazima uzijue ili kuanza kusonga mbele na kupiga hatua katika maisha.
Kila sababu hizi za mafanikio ni sababu za msingi zinazobadili maisha ya mtu kwenda katika mafanikio makubwa, pindi utakapozitendea kazi sababu hizi katika maisha yako utapiga hatua katika kila jambo utakalolifanya ma kufanikiwa katika maisha. Twende pamoja tuziangalie sababu hizi ili kufikia mafanikio makubwa.
Elimu (Education)
Sababu ya kwanza itakayokufanya upige hatua kufikia mafanikio ni elimu. katika jamii zetu watu waliofanikiwa sana ni watu wanaojua mambo mengi kuliko watu wa kawaida, wanajua kiundani juu ya jambo fulani kuliko watu wa kawaida, hivyo matokeo yake wanatumia ujuzi huo kutengeneza thamani na nidhamu katika jambo wanalolifanya. Sheria ipo hivi "ukitaka kufanikiwa sana, jifunze sana" kama unataka kuongeza kipato chako na kufanikiwa katika maisha yako ni lazima uongeze kiwango chako cha uelewa juu ya jambo unalolifanya mfano biashara soma sana kuhusu soko, ubora wa bidhaa, namna ya kupata wateja zaidi nk.
Ujuzi (skill)
sababu ya pili itakayokufanya upige hatua kufikia mafanikio ni ujuzi. Uwezo wako katika jambo fulani ndio utakaoleta matokeo, kwa namna utakavyojitoa katika kitu unachokifanya ndivyo utakapopata matokeo. tumia ujuzi wako katika jambo unalolifanya. Kwa namna utakavyoongeza ujuzi katika kitu unachokifanya kwa kusoma au kwa uzoefu utapata matokeo makubwa katika jambo utakalolifanya. tumia ujuzi wako katika kufanya jambo unalofanya na utapata matokeo makubwa na kufanikiwa.
Mawasiliano (contacts)
Sababu ya tatu inayokufanya kukua na kufikia mafanikio makubwa ni mawasiliano. kwa kila mabadiliko yanayotokea katika maisha yako yanategemea unahusiana na watu gani, kufanikiwa kwako kunategemea watu wanahusiana na wewe wanaokupenda na wanaotamani ufike mbali na wanakusaidia. Angalia watu unaohusiana nao acha kuhusiana na watu wenye mtazamo hasi daima watakwamisha safari yako ya mafanikio, wahenga wanasema "mafahari wawili wanakaa zizi moja" achana na watu waliokata tamaa, ongozana na watu wenye mawazo ya ushindi na kila siku wanataka kukuona ukifanikiwa.soma zaidiHakuna kinachoshindikana kama ukiamua
Taswira nzuri (positive image)
sababu ya nne itakayokufanya upige hatua kufikia mafanikio makubwa ni taswira nzuri. watu wanakuelezea wewe kwa namna unavyoonekana kwa nje, kwa namna unavyoonekana. Ukweli uko hivi unamwelezea kila mtu kwa namna anavyoonekana katika jamii, hivyo jitahidi kuwa na muonekano utakao wavutia watu wengi kufanya kazi na wewe na hivyo kupiga hatua kuelekea mafanikio makubwa, chukua muda tathmini namna unavyoongea, unavyovaa, unavyotembea na kila kitu, hakikisha mtazamo wako unaendana na kile unachokifanya hii itawavutia wengi kufanya kazi na wewe. soma zaidi Sheria ya mvuto (law of attraction)
Ubunifu (Creativity)
Ubunifu ni njia pekee itakayokufanya upige hatua katika jambo unalolifanya na kufanikisha malengo yako. Watu wengi sana wamapenda kuiga jambo analolifanya mtu mwingine hivyo kujikuta kila siku anapiga hatua kurudi nyuma na hivyo kukata tamaa. Ubunifu ndio zana pekee itakayokufanya ukuze kitu unachokifanya, mfano kama unafanya biashara au unataka kuanzisha biashara buni kitu cha kipekee au ongeza ubunifu pale ambapo wengine hawajaweka hapo utapata matokeo makubwa katika jambo ambalo unalifanya.
Nakushukuru kwa kuwa pamoja nami fanyia kazi sababu hizo na utapiga hatua, hutabaki kama ulivyo.