MAKALA: HAKUNA KINACHOSHINDIKANA KAMA UKIAMUA

Habari za muda na wakati mpendwa rafiki yangu, nakukaribisha tena kwa mala nyingine kujumuika pamoja nasi kushirikishana mbinu mbalimbali za mafanikio. Rafiki lengo kuu la mtandao wa Rise Africa ni kufundisha na kuona kila kijana wa kiafrica amefanikiwa hii ni kwa sababu hakuna aliyezaliwa na mafanikio sio tajiri wala sio masikini wote tumezaliwa sawa na wote tumepewa uwezo mmoja pasipo kupendelea lakini kinachotofautisha waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni namna ya kutumia huo uwezo tuliopewa. Leo napenda tuangalie kitu kikubwa katika mafanikio hakuna kinachoshindikana kama ukiamua.
Watu wengi sana wanapenda sana kuwalaumu watu wengine kwamba ndio wanaokwamisha wao wasifanikiwe, utasikia wengine wanailalamikia serikali haijawapa ajira, wengine wanawalaumu ndugu, jamaa na marafiki kwamba washindwa kuwaunganisha katika kazi mbalimbali hivo kujikuta wako pale pale. mpendwa rafiki swala hili halina ukweli hata kidogo wewe mwenyewe ndio mwenye maamuzi ya mwisho juu ya maisha yako, wewe mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kuamua ufanikiwe au usifanikiwe, hivo ulivyo sasa hivi ni matokeo ya kile ulichokiamua.
 Mpendwa rafiki katika maisha yako kuna njia mbili njia ya mafanikio na njia ya kutokufanikiwa sasa uamuzi uko mikononi mwako, wewe mwenyewe ndio mwenye maamuzi ya njia ipi nipite, hivo usimlaumu mtu kwa kutokufanikiwa kwako kwa maana hivyo ulivyo leo ni uamuzi wako mwenyewe. Biblia inasema Kuna njia mbili machoni pa mwanadamu njia ya uzima na njia ya mauti hivo ni maamuzi yako upite njia gani inayokufaa wewe.
Related image
Mpendwa rafiki hebu twende tuangalie ni kwa namna gani ufanye maamuzi sahihi yatakayokuletea mafanikio:-
Tafakari ni nini hasa unachokipenda
Mpendwa rafiki kila mwanadamu ameumbwa na kitu anachokipenda na akikifanya huwa anakifanya kwa umakini na kumletea furaha na mafanikio, kila mtu anacho kitu anachokipenda ila wengi wetu hatujui ni kitu gani unachopenda kukifanya zaidi na kujikuta tunafanya kazi ambazo hatuzipendi na kukosa ubunifu na kujikuta tunakuwa pale pale kila siku, sasa kujua unapenda nini chukua karatasi na kalamu anza kuandika vitu vyote unavyovipenda kufanya zaidi na ukifanya utafanya kwa ufanisi mkubwa, kila kazi unayoiandika ipe namba kuanzia moja na kuendelea hakikisha unapanga kwa kupenda zaidi basi ile  namba moja ndiyo unayoipenda zaidi sasa chukua hatua tumia kitu hicho fanya kwa ufanisi mkubwa utafanikiwa.
Amua kupanga mipango yako na uiandike.
Mpendwa rafiki amua leo kupanga mipango yako na uiandike sehemu ambayo utaipitia kila siku kufanya hivi kutakutengenezea tabia ya kufuatilia mipango yako na kujua ni namna gani uanze kuitekeleza, kwa mfano  unataka kufanya biashara panga mpango ni biashara gani unataka, unataka uanze lini hiyo biashara inagharamu kiasi gani yaani andika kila kitu.
Amua kuweka juhudi katika jambo unalolifanya
Mpendwa rafiki amua leo kutokufanya kazi kwa ulegevu, mafanikio sio kitu rahisi kinahitaji watu waliojitoa na kupigania kufanikiwa, amua kuacha kulala  sana, mpendwa rafiki watu waliofanikiwa ni watu wanaoamka mapema na kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa, mpendwa rafiki weka juhudi kubwa sana katika jambo unalolifanya mpaka likupe mafanikio, Tukitazama Biblia Yesu anasema " Kwa maana kila aombae hupokea na atafutae atapata na abishae atafunguliwa", hivo tunaona ata katika mafanikio ukiweka juhudi kubwa ni lazima ufanikiwe.
Amua kutokupoteza muda
Mpendwa rafiki watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwa sababu wao wenyewe wanapoteza muda, Muda ni zawadi kubwa sana aliyotupatia Mungu ukiitumia vema utafanikiwa, mpendwa rafiki kataa watu wanaokupotezea muda wako tambua muda wako ni wa thamani sana na hapa duniani upo kwa muda tu hivo utumie muda wako vizuri ili kupata mafanikio, acha kutumia muda wako mwingi kuongelea watu, kujadili siasa badala ya kufanya kazi, amua kutumia muda wako vema na utafanikiwa.
Image result for time wasters photos
Amua kuachana na watu waliokata tamaa
Mpendwa rafiki amua kuachana na watu waliokata tamaa, unajua katika maisha watu waliokata tamaa wanapenda sana kumkatisha tamaa mtu mwingine, mfano mtu alishindwa kuingia katika biashara fulani utasikia anamuambia mtu anaetaka kuianza kwamba hutoiweza hiyo biashara, na pia hawa ni watu wanaopenda kuongelea wengine mala nyingi utawakuta wamekaa wanazungumza habari za wengine hivo amua kuachana nao kabisa ambatana na watu wanaoamini katika mafanikio hawa watakupa msukumo mkubwa wa kukufanya uweke juhudi kubwa sana katika mafanikio.
Naamini umeelewa mpendwa msomaji na utachukua hatua kwani maamuzi ni ya kwako kufanikiwa au kutokufanikiwa katika biblia Mungu anasema "mbele yako kuna uzima na mauti, chagua uzima upate ishi", hivo nami napenda kukuambia kwamba mbele yako kuna mafanikio na kutokuwa na mafanikio nakushauri chagua mafanikio ili uwe na furaha na amani katika dunia hii. Nikutakie siku njema mpendwa rafiki.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email            : fanuelmwasyeba@gmail.com