Habari ya siku mpendwa msomaji wa makala za Rise Africa ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya, karibu tena hapa hapa tunapokutana kujadiliana na kushirikishana mambo mbalimbali yahusuyo mafanikio, hapa hakuna tunachoongelea kingine zaidi ya mafanikio kwa maana nia yetu na malengo yetu ni kufanikiwa.
Nakukaribisha katika makala yetu ya leo ambapo nataka tuangalie kwa jicho pevu mambo ambayo kwa namna moja au nyingine unapaswa kuachana nayo kama unataka kufanikiwa, unajua rafiki kila siku nakuambia mafanikio sio jambo rahisi wala lele mama ni jambo linalohitaji kuachana na tabia zako za awali na kufata tabia za kimafanikio ambazo bila kukubali mwenyewe toka moyoni huwezi.
naamini mpaka unasoma makala zetu basi najua umedhamilia kufanikiwa na nakupongeza kwa hilo ila ukitaka kufanikiwa kweli acha tabia zako za awali ambazo zimekufanya uwe hapo ulipo mpaka leo.
Sasa twende pamoja tuangalie ni vitu gani unapaswa kuachana navyo kama unataka mafanikio:-
Acha kufanya kitu bila malengo
mpendwa rafiki watu wengi waliofanikiwa waliweka malengo na matarajio ya muda mrefu na malengo hayo wameyaandika hii inajenga picha na namna utakavoanza kufanya mikakati yako, hivo mpendwa msomaji acha kufanya mambo bila malengo, huwezi kufanikiwa bila kuwa na malengo, malengo ndiyo dira kuu inayokuelekeza wapi uende na nini ufanye kwa wakati gani, hivo anza kuweka malengo na ni lazima malengo hayo yaandikwe na yawe na muda ili kukufanya ufanye kazi kwa muda muhafaka.
Acha kufanya mambo kwa mazoea.
Mpendwa rafiki watu wengi wanapenda kufanikiwa na mwanzo kabla hawajaanza huwa na hamasa kubwa sana ya kufanya jambo mfano biashara lakini pindi anapoianza biashara basi hujikuta anaijengea mazoea na kuacha kufanya kazi kwa ufanisi na kujikuta ana biashara lakini bado yuko pale pale, mpendwa rafiki kufanya jambo kwa mazoea ni mbaya na ni sumu kwa mafanikio. watu waliofanikiwa kila siku upenda kujifunza jambo jipya kutokana na kile anachokipenda na hivo kujikuta kila siku anakuwa mbunifu na kuifanya biashara yake kuwa kubwa zaidi kwa kadri siku zinavoenda, hivo mpendwa rafiki kama unataka kufanikiwa hebu achana na kufanya kazi kwa mazoea, weka juhudi na ufanisi katika jambo unalolifanya utafanikiwa.
Acha kujiona huwezi kufanya mambo makubwa
Mpendwa rafiki watu wengi wanapendwa kujiona wadhaifu hawawezi kufanya mambo makubwa, mfano utasikia mtu anasema, "sisi hatuna uwezo wakufanya biashara hizi bwana sisi biashara zetu ni hizi hizi za kina kabwela", mpendwa rafiki hii ni hofu waliyonayo watu wengi na kujikuta wanafanya mambo madogo miaka yote bila kusonga mbele, rafiki kile ukiamuacho ndiyo hatima yako kama umeamua kufanya mambo madogo basi huwezi fikia kufanya mambo makubwa, watu waliofanikiwa ni watu wanaojiamini na kujikubali kuwa wanauwezo wa kufanya mambo yote ya kimafanikio bila kizuizi chochote hivo kama jambo halijui hutia nia na kujifunza juu ya jambo hilo na kulifanyia kazi na kujikuta wakifanikiwa. Hivo mpendwa rafiki acha kufanya mambo madogo madogo waza kufanya mambo makubwa yatakayokuletea mafanikio.
Acha neno samahani/kujitetea
Mpendwa rafiki hakuna kitu kinachowafanya watu wasifanikiwe kama neno samahani, unajua neno hili linatumika vibaya mfano mtu kapatiwa kazi afanye muda huu utasikia anasema samahani nitafanya muda mwingine, mpendwa rafiki acha kujitetea wengine utawasikia haa hizi kazi ni za kike au za kiume hivo sifanyi, mambo haya yamewafanya watu wengi wabaki kama walivyo siku zote. w atu waliofanikiwa hawapendi kujitetea hufanya kazi muda wowote na kuikamilisha kwa wakati hivo wanafanikiwa, mpendwa rafiki acha kujitetea kumbuka hayo ni maisha yako na muamuzi wa maisha yako ni wewe mwenyewe weka juhudi katika kazi utafanikiwa.
Acha kulalamika/kulaumu
Mpendwa rafiki watu ambao hawajafanikiwa hupenda sana kulalamika, yaani katika kila jambo lake lisipokwenda sawa basi atalalamikia wengine kwamba ndio wamefanya asifikie mafanikio, mpendwa rafiki ulalamishi sio dawa na wala sio kitu kitakachokupa wewe mafanikio zaidi ya kukufanya uwe hivo hivo kila siku, Katika Biblia Mungu mwenyewe anachukia kulalamika mfano alipokwenda bustani ya Eden akamuuliza Adamu " nani kakuambia u uchi Adam akasema Bwana ni huyu mwanamke uliyenipa ndiye amenipa tunda lile ulonikataza", ukitazama Adm na Eva waliadhibiwa na Mungu kwa sababu ya kutokukubali kosa na kubaki wakilaumu, hivo lawama hazitakupeleka popote weka nia na malengo thabiti pambana mpaka mwisho utafanikiwa.
Baisi naamini umejifunza kitu nakuchukua hatua ya kuacha vitu hivyo, kila siku nasisitiza kwamba wwe ndiye mwenye maamuzi ya mwisho uchague mafanikio au uendelee kuwa hivo hivo ulivyo, kumbuka mafanikio ni haki ya kila mmoja. Nakutakia siku njema mpendwa rafiki.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano : 0717262705/0683636572
Email : fanuelmwasyeba@gmail.com