FIKRA PEVU 1: HILI NDILO ZOEZI LITAKALOBADILISHA MAISHA YAKO

Habari yako mpendwa rafiki natumaini u mzima wa afya, karibu tena katika ukurasa wetu ambapo tunakutana kujadili mambo mbalimbali yahusuyo mafanikio, kila siku napenda kumuona kila kijana wa Africa amefanikiwa. Mpendwa rafiki watu wengi wanapenda kubadilisha maisha yao kufikia mafanikio makubwa lakini wanajiuliza watafanyaje ili wabadilishe maisha yao, ili ni swali kubwa sana ambalo watu wengi sana wanaopenda kufanikiwa wanajiuliza "ninapenda kufanikiwa, ila sijui nianzie wapi au nianze vipi?", twende pamoja.
Hili ndilo zoezi litakalobadilisha maisha yako na kufanikisha malengo yako, hili ni zoezi rahisi na lenye nguvu sana katika kufanikisha malengo. Chukua kipande cha karatasi na orodhesha mambo kumi unayotaka kuyakamilisha kwa miezi kumi na mbili ijayo. Andika  malengo hayo katika wakati uliopo mpaka mwaka upite na kuhakikisha tayari umeyafanikisha.Soma zaidiHow to win your goal

Tumia neno "ni" katika kila lengo kuonesha umiliki mfano "nimeingiza milioni tano kwa mwaka", "nimefanikiwa kupanua biashara yangu kufikia mtaji wa laki tano". Hii inaenda kutengeneza kwenye ufahamu na msukumo mkubwa wa kutimiza malengo hayo.

Hili ni zoezi la ajabu sana, pengine ni kama muujiza, lakini kama ukifanya kuandika malengo yakokumi katika karatasi na ukaliweka kando kwa mwaka, baada ya miezi kumi na mbili ukienda kulipitia na kuitazama orodha ya malengo utakuta malengo nane kati ya kumi umetimiza. chukua hatua sasa badilisha maisha yako kufikia mafanikio makubwa. soma zaidiHakuna kinachoshindikana kama ukiamua

Mpendwa rafiki fanyia kazi zoezi hili na unapokwama naomba unishirikishe kuona ni namna gani ya kufanya, narudia tena uamuzi wa kufanikiwa ni wa kwako binafsi, wewe ndie mwenye kuamua uwaje katika hii dunia. Bill Gates  ameshawahi kusema "kuzaliwa masikini sio kosa lako, bali kufa masikini ni kosa lako". Chukua hatua sasa.
                                  Your choice,your life
Mwandishi; Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano; 0717262705/0683636572
Email            ; fanuelmwasyeba@gmail.com