MAKALA: UHUSIANO WA MAISHA NDEGE TAI NA MAFANIKIO

Habari za muda huu mpendwa rafiki yangu nafurahi kukutana na wewe siku ya leo tena katika kushirikishana mambo mbalimbali yanayohusu mafanikio, lengo la mtandao wa rise africa ni kuona kila kijana wa kiafrika amefanikiwa hivyo hatutachoka kushirikishana mbinu na namna ya kuyafikia mafanikio. Leo napenda nikushirikishe siri za mafanikio kupitia ndege tai, ukiangalia taifa la marekani katika bendera yake ipo picha ya ndege tai, hivi umeshawahi kujiuliza ni kwanini walimuweka tai na si wanyama au ndege mwingine?, jibu ni kwamba tai anasifa za kipekee ambazo wanyama au ndege wengine hawana ni ndege lakini ana nguvu sana hivo kutokana na sifa zake za msingi taifa la marekani likaamua kujifananisha na ndege tai.
Tai ni moja kati ya aina ndege walio maarufu, Umaarufu wake umejikita katika mtindo wake wa maisha ambao ni wa kipekee.
Kuna aina nyingi wa Tai mfano; kuna tai mwenye mkia mweupe, kuna tai mwenye rangi ya dhahabu, kuna tai wa Ufilipino na kadhalika. Inakadiriwa kufikia aina sitini za tai duniani na wengi wao wanaopatikana Afrika, Ulaya na Asia.


Tai ni ndege aliye na sifa za upekee hasa kutokana na ufundi wao wa kuwinda, uwezo wao wa kuona kwa macho ni mzuri kwa sababu anaona Umbali mara saba zaidi ya jinsi anavyoona binadamu. 

Tai hukadiriwa kuweza kuishi zaidi ya miaka 60 na pindi afikishapo miska 50 makucha yake huwa yanakuwa yameshachoka, mdomo wake nao huisha makali. 

SASA TWENDE TUONE UHUSIANO WA MAISHA YA NDEGE TAI NA MAFANIKIO

1 Tai hupaa juu sana angani wala shomoro na kunguru hawawezi kufika huko. Hakuna ndege yeyote mwenye uwezo wa kupaa juu sana kufikia kimo anachofikia tai.  Mara nyingi huwa tunawaona mwewe wakipita sehemu fulani, shomoro na kunguru huwazomea lakini tai hataki ujinga huo yeye huruka anga la juu kabisa.
FUNZO: kuwa na mipango mikubwa sana mpaka watu wengine qwashangae umewezaje kupanga mipango mikubwa hivo, pia ishi na watu wenye mitazamo chanya na mafanikio, acha kupoteza muda na watu waliokata tamaa ya maisha ya mafanikio nenda kwa wenye mipango mikubwa wenzako. Tai huruka na tai wenzie.

2 Tai wanauwezo wa kuona mbali sana. wana uwezo kuona kitu kilichoko umbali wa kilometa tano. Tai akiona mawindo yake huangalia pale pale na huanza kwenda kukamata mawindo hayo kwa kasi kubwa. Haijalishi kama kuna vipingamizi vyovyote njiani, tai hatabadili kuangalia mawindo yake hadi akamate mawindo.

FUNZO: Unatakiwa kuwa na maono na uyatazame mpake uyapate au uyatimize hiyo ndio siri ya kuelekea mafanikio yako, watu wengi wana maono na malengo makubwa lakini panapotokea vikwazo basi huyaacha malengo yake na kujikuta yuko pale pale, haijalishi vikwazo unavyokumbana navyo njiani, wewe kaza mwendo bila kurudi nyuma kufikia malengo na matarajio yako.

3 Tai hali mzoga, anakula kile tu alichokamata yeye, tai hali kitu ambacho hajawinda yeye, tai huamini kile alichokiwinda yeye ni bora zaidi hivo ata kama ana njaa kiasi gani hawezi kula mzoga yaani ni bola alale njaa kuliko kula mzoga.

FUNZO: Watu wengi siku hizi wanapenda kusikiliza mambo ya watu, wanapoteza muda mwingi kusikiliza redio au runinga ili kusikiliza mambo ya wengine au utakuta wengine wanakaa mpaka chini kumsema mtu mwingine au kufuatilia maisha ya wengine na kujikuta mambo ya msingi hawayafanyi na kubaki masikini. Kuwa makini na kile unacholisha macho yako, masikio yako hasa kuangalia filamu na luninga. Usipende kutumia mizoga (mambo machafu) kwa sababu utaiharibu nafsi yako na maisha yako hayatakwenda kwa kasi kubwa ya mafanikio.

4 Tai wanapenda mvua kubwa na yenye upepo. Mawingu yakikusanyika tai wanafurahi. Tai hutumia upepo wa mvua kupaa juu sana hatumii nguvu nyingi kupaa anaweza kutandaza tu mabawa yake halafu anaanza kuelea bila shida akifurahia maisha mazuri. Huku ndege wengine wakati wa mvua kubwa yenye upepo hujificha kwenye mapango.

FUNZO:
watu wengi wanaogopa na kuyakimbia matatizo na changamoto na kujikuta wanashindwa na kukata tamaa kuhusu mafanikio.Tunaweza kutumia mvua kubwa yenye upepo(changamoto) kujinyanyua juu sana watu wote waliofanikiwa wengi wao hufanikiwa wakati wa changamoto kubwa. Wao hutumia mvua ya upepo kupaa juu sana angani tena wakati mwingine juu ya mawingu. Tumia matatizo kama changamoto inayokutoa toka sehemu moja kwenda nyingine, 

5 Tai hupima kwanza kabla ya kuamini. Tai jike akitaka kukutana na tai dume na wakataka kujamiiana, tai jike hupaa kwa kasi kubwa kwenda chini wakati huo tai dume anafuatia kwa nyuma. Akifika chini huchukua tawi la mti kisha hupaa tena angani na tawi hilo huku tai dume anafuata kwa nyuma. Akifika umbali mrefu angani tai jike huliachia hilo tawi na tai dumr hulikimbilia mpaka alikamate kabla halijadondoka chini na akisha likamata analirudisha tena juu kwa tai jike. Tai jike atalipokea hilo tawi na anapaa nalo juu sans halafu analidondosha tena. Kama kawaida yake tai dume atalifukuzia mpaka alikamate na atalirudisha kwa tai jike tena. Tai jike ataendelea na mchezo huu mpaka ajirizishe kwamba tai dume huyo yuko vizuri na amefuzu majaribio hayo. Hapo ndipo tai jike atakubali kupandwa na tai dume huyo jike.

FUNZO: Katika maisha yako binafsi au katika biashara au katika mapenzi yako, unatakiwa kupima mtu unayetaka kumpenda au kushirikiana naye kama kweli ana dhamira ya dhati au ni muigizaji tu. Kabla ya kumpa mtu fursa ya kumuamini na kufanya nae kazi anza kumjaribu ili umuone ana uvumilivu wa kiasi gani katika jambo mnalotaka kulifanya ili kupata mafanikio.

6 Tai akitaka kutaga mayai, tai jike na tai dume hushirikiana
Tai akitaka kutaga mayai, tai jike na tai dume hushirikiana kutafuta sehemu iliyo juu sana kwenye mti ambayo sehemu hiyo haina maadui. Kisha tai dune anaenda chini ardhini kuchukua mitu yenye miiba anakuja anaitandaza kwenye sehemu wanayotengeneza kiota. Tai dume tena hurudi ardhini kuchukuwa matawi ya mitu kwa ajili ya kutengeneza kiota kikubwa. Kisha baada ya kuweka miiba na vimatawi vidogo vya mti, tai huyu anaenda tena chini kuchukua majani laini, akimaliza kuweka majani laini anatudi tena kuchukua miiba anakuja anaiweka juu ya kiota ili kuzuia maadui na mwisho akimaliza hayo yote ana nyonyoa baadhi ya manyoya yake ili kuweka sehemu ya mayai. Wanasaidiana na tai dume kuyaatamia kwa zamu, pia kazi ya ulinzi huifanya wote kwa kushirikiana. Vifaranga wakishatotolewa; tai dume na tai jike hushirikiana kuwalea. Baada ya muda kidogo tai jike ataanza kuwatoa vifaranga na kuwaweka kwenye miiba pembeni kidogo ya kiota, halafu vifaranga hurudi ndani ya kiota, atafanya hilo zoezi mara kadhaa baadaye atayaondoa manyoya kwenye kiota. Wale watoto wakirudi kwenye kiota watakutana na miiba itawachomachoma na kuvuja damu. Kisha tai jike atawarusha chini wale vifaranga kabla hawajadondoka tai dume atawadaka ataendelea na zoezi hilo moaka watoto wafahamu kuruka.

FUNZO: Pale tai wanapoandaa kiota wanatufundisha kujuandaa kwa ajili ya mabadiliko. pia hapa tunajifunza kabla ya kufanya jambo lolote ni lazima tuweke mipango kwanza, mipango ndiyo itakayotufanya tufanikiwe, pia ushirikiano katika kutimiza jambo fulani ni muhimu sana, hakuna mafanikio bila kuwa na ushirikiano, shirikiana na watu wengine wenye malengo hapo utapata mawazo mapya na namna ya nini ufanye ili kuepuka changamoto hapo utafanikio.


7 Tai anapozeeka, manyoya yake huwa dhaifu na hayatamwezesha kupaa kwa kasi kama hapo zamani. Akiona hivyo huenda kwenye pango mbali na maadui, akifika humo kwenye pango hujinyonyoa manyoya yote hadi anabaki uchi kabisa. Anaendelea kujificha humo mpaka anaota manyoya mengine ndipo anatoka nje.

FUNZO:Wakati mwingine tunatakiwa kuziacha baadhi ya tabia mbaya ambazo zinatukwamisha kufikia mafanikio yetu makubwa. ukipata changamoto katika safari ya mafanikio kamwe usikate tamaa nenda kajipange upya na urudi kwa kasi na utafanikiwa tu.
nakutakia siku njema mpendwa rafiki pambana kupata maisha bora.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email            : fanuelmwasyeba@gmail.com

1 comments: