habari ya asubuhi rafiki yangu mfuatiliaji wa mtandao wetu wa rise africa ni matumaini yangu u mzima wa afya, karibu katika siku nyingine tena kushirikishana mambo mbalimbali yahusuyo mafanikio, mpendwa rafiki rise africa tumedhamilia kufanikiwa kwa sababu Binadamu wote tumezaliwa sawa wote tumepewa ufahamu sasa kwanini wengine wafanikiwe na wengine washindwe kufanikiwa kumbe hapa tunaona kwamba suala la kufanikiwa au kutokufanikiwa ni la mtu binafsi hivo hivo tunaamini katika kuthubutu na kutenda kwa nidhamu ndiyo siri ya mafanikio yetu, bilionea wa kwanza duniani anasema " kuzaliwa masikini sio kosa lako bali kufa masikini ni kosa lako".
Mpendwa rafiki kila mmoja wetu hapa duniani anapenda maisha bora na yenye mafanikio makubwa ndiyo maana ukiimuuliza mtu yeyote anataka nini katika maisha yake atakuambia mafanikio lakini swali ni kwamba kwanini watu wanashahuku kubwa ya kupata mafanikio lakini hawayapati inabaki kama stori tu?, leo napenda nikushirikishe ni kwanini watu wengi wanapenda mafanikio lakini hawayapati karibu:-
watu wengi sana hawafanikiwi kwa sababu wanatenda kinyume yaani kile akipendacho hakitendi bali kile hasichokipenda ndicho anakitenda. mpendwa rafiki watu wemgi wanampenda Mungu na wanapenda waje kufika mbinguni lakini cha kushangaza hawayatendi yale yampendezayo Mungu, pia watu wote wanajua madhara ya kuwa na wapenzi wengi ni kupata magonjwa ya zinaa lakini cha kushangaza watu wanaendelea kuwa na wapenzi wengi licha ya kujua madhara yake.
Mpendwa rafiki kila mtu anajua uvivu ni adui mkubwa wa mafanikio lakini watu wanazidi kuwa wavivu huku wakitarajia mafanikio kitu ambacho hakiwezekani. mpendwa rafiki naamini hadi hapo umeeelewa kuwa watu wengi wanatenda yale wasiyoyapenda na yale wayapendayo hawayatendi, sasa twende tuone ni kwa namna gani tufanye yale tuyapendayo ili kupata mafanikio:-
1 Weka mipango na uisimamie.
rafiki yangu katika suala la mafanikio mipango ndiyo ufunguo wa mafanikio,huwezi kufanikiwa kama huna mipango,mwanadamu hajaumbwa afanye kila kitu bali ameumbwa kufanya jambo la muhimu zaidi,kamwe huwezi fanya kila kitu na ukifanya hivo ni mwanzo wa kufeli katika maisha,katika kuweka mipango kunakufanya ufanye mambo yaletayo mafanikio tu na kuachana na mambo ambayo yanakufanya ubaki vile vile kila siku. Katika kuweka mipango ni lazima uweze kupanga ratiba yako,kabla hujachagua nini cha kufanya tathmini kwanza malengo yako,Brian Tracy katika kitabu chake cha eat that flog anatuambia " think on paper",malengo yako usiyaache kichwani yaandike ili kila ukiyaangalia yakupe hamasa ya kusonga mbele.
2 Kuwa na nidhamu katika kila jambo.
mpendwa rafiki nidhamu ndio nguzo kubwa ya mafanikio usipokuwa na nidhamu wewe na mafanikio hamuwezi kuendana, ukishaweka mipango na mikakati sasa weka nidhamu katika hayo mpaka yakamilike, watu wengi wameshindwa kupata mafanikio kwa sababu wamekosa nidhamu basi wanajikuta wanatenda yale ambayo hawayapendi, mpendwa rafiki unapaswa kuwa na nidhamu ya muda ambayo unapaswa kuujali muda vema kwa sababu muda ukipita haurudi tena hivo ukiipata siku tambua umepewa siku hiyo tu kufanya mambo yako hivo ukiitumia vibaya basi sahau mafanikio, kuwa na nidhamu ya fedha, mpendwa rafiki hapa kwenye fedha kuna changamoto kubwa watu wengi hawana nidhamu ya fedha wanatumia zaidi kuliko wanachoingiza hivo kujikuta wako pale pale kila siku hivo rafiki hebu jenga kutumia fedha zako kwa nidhamu weka akiba ili kujenga mafaniko yako.
3 Tambua thamani ya jambo unalolifanya
Rafiki watu wengi tunafanya jambo bila kujua thamani ya jambo hilo maishani mwetu, kujua thamani ya jambo ni njia njema ya kulifanikisha jambo hilo, mfano kama tungekuwa tunajua kwamba mafanikio ndiyo yatakayotufanya tuishi kwa furaha na kupata kile tunachokitaka hakuna ata mmopja wetu ambae angeacha kufanya mambo muhimu. hebu chukua muda na tafakari ni jambo gani lina thamani kubwa sana kwako ambalo ukilifanya linaleta mabadiliko chanya katika maisha yako, ukilitambua usipoteze muda anza kulifanyia kazi na utafanikiwa.
4. Tambua kipaji au kipawa chako
Rafiki watu wengi wanafanya yale wasiyoyapenda kwa sababu ya kukosa kujua wana kipaji au kipawa gani, ni muhimu kujua kipaji chako, ukijua tu ni mwanzo wa kufanya kile unachokipenda na kuanza kukupa mafanikio, watu wengi wanauliza watawezaje kutambua kipawa au kipaji chako sasa fanya hivi kaa sehemu tulivu anza kutafakari ni kitu gani unakipenda sana kuliko vyote na ukipata nafasi ya kukifanyia kazi basi utafanya kwa ufanisi mkubwa?, katika kutafakari huko basi utapata jambo ambalo ndio kitu Mungu amekupa kamza zawadi ya kwanza ya mafanikio itumie vema kupata mafanikio.
5 Penda kujifunza juu ya jambo unalolipenda.
Rafiki watu wengi wanafanya vitu wasivyovipenda kwa maana vile wanavyovipenda hawana uelewa mkubwa sana juu ya jambo hilo, hivo kujikuta wakikata tamaa na kufanya mambo wasiyoyapenda, mfano mtu anapeenda biashara lakini hana ujuzi juu ya biashara hivo kunamfanya akate tamaa na kujikuta anaacha lengo lake na kufanya mambo asiyoyapenda. Penda kujifunza kila siku jambo jipya juu ya kile unachopenda hii itakufanya uwe bora na mwenye ufanisi mkubwa juu ya jambo unalolipenda, mfano unaweza kujifunza kupitia makala za kimafanikio kupitia mitandao mbalimbali kama vile Rise Africa na mingineyo, kusoma vitabu au kusikiliza vitabu vilivyowekwa kwa njia ya sauti ili kupata ujuzi zaidi juu ya jambo unalolipenda.
6 Kuwa na maono
Rafiki watu wengi hawana maono kwamba wanataka kuja kuwa nani au wakishaondoka hapa duniani wataacha alama gani, hivo kujikuta wanarizika na kufanya yale mambo wasiyoyapenda. Maono yanatufanya tufanye yale mambo ambayo yatakamilisha maono yetu, maono ni kama dira inayotutaka tufikie sehemu fulani. hivo tunafanya juhudi kubwa ili kufikia pale tunapopataka, mfano mimi napenda na natarajia kuwa bilionea sasa katika kufikia hili sipendi kupoteza muda au fursa inayokuja mbele yangu. Hivo mpendwa rafiki ili upate msukumo wa kufanya mambo unayoyapenda ni lazima uwe na maono ambayo yatakufanya ufanye mambo ambayo yatakamilisha maono yako.
kwa leo tuishie hapo najua kwa namna moja ama nyingine umejifunza jambo ili kufanya yale mambo tuyapendayo na kuachana na mambo ambayo hatuyapendi na yanatukwamisha sana katika kutaka kufanikiwa. Nikutakie siku njema na endelea kuwa nasi kila siku kupata mafunzo mbalimbali nina imani kubwa kwamba huwezi soma makala za Rise Africa na ukabaki pale pale, lengo na nia yetu ni kufanikiwa na lazima tufanikiwe. Asante
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email : fanuelmwasyeba@gmail.com