Habari ya muda huu mpendwa msomaji wa makala za riseafrica ni matumaini yangu u mzima wa afya karibu tena tushirikishane mambo ya msingi kwa mafanikio yetu, leo naomba tujifunze nguvu ya msamaha katika kupata mafanikio, mpendwa rafiki mwanadamu ameumbwa akiwa na mapungufu hakuna mkamilifu katika dunia hii, hivo kukoseana ni jambo ambalo halipingiki, watu wengi hatulijui hili basi mtu akikosea basi ndio unamjengea visasi na kujikuta tunapoteza muda mwingi katika kushughulika na visasi na kuacha kushughulika na mambo yanayoweza kutupatia mafanikio.
Tungeweza kutambua kwamba mtu anakosea huenda sio lengo lake bali chanzo ni udhaifu wa kibinadamu ambapo ata wewe umewakosea wengine kwa sababu na wewe ni binadamu hujakamilika, hivo kupishana mala nyingi ndio tunapojifunza hivo msamehe mtu aliekukosea na usimuweke moyoni ili uendelee na kazi zako nyingine za kimafanikio kuliko kupoteza muda mwingi kumfikiria mtu na kuacha mambo yako ya msingi.
Katika tafiti ambazo zimewahi kufanywa na wanasaikolojia miaka ya nyuma, waligundua ya kwamba watu wengi hawana maendeleo yao binafsi kwa sababu hawatambui nguvu ya msamahama iliyovyo na nguvu katika safari ya Mafanikio. Tafiti hizo hizo zinaendelea kusema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wamebeba mizigo mizito ndani nafsi zao.
Mizigo hiyo mizito ambayo inawezekana kuna mtu alisabibisha mtu kuwa katika hali hiyo. Kwa mfano inawekana kuna ndugu,rafiki, mzazi aliwahi kukukosea ambapo anafanya usimsahau na kuamua kutaka kulipiza kisasi. Maneno au vitendo hivyo vimekusababisha kwa kiasi kikubwa upunguza hamasa za kiutendaji, magonjwa na mawazo mengi (stress).
Hebu tuangalie japo kwa uchache ni kwa kiasi gani madhara ya kutokusamehe yanavyoweza kukuathiri. Msipo msamehe mtu kunakupekea kwa kiwango kikubwa kuweza kupunguza uwezo wa kufikiri vitu vipya, chuki, visasi, mauaji, magonjwa ya moyo (BP), hata hivyo pamoja na kupunguza uwezo wa kufikiri kunakupelekea kuzama katika dibwi kubwa la mawazo, hata hivyo mawazo hayohayo yanakupekea kujikita katika tabia zisizo za kimaadili kwa mfano ulevi, wizi na mengineyo mengi.
Basi bila kupata kigugumizi cha kusoma makala hii hebu jaribu kusoma kwa umakini na uingie katika kilindi cha nafsi yako harafu jiulize umebeba vitu gani juu ya watu wengine? Kisha jaribu kutafakari kwa umakini tena mambo hayo yamekuathiri kwa kiwango gani?, jiulize ni mambo mangapi ya msingi uliyoyaacha tangu umeweka visasi vyako ambayo yangekutoa hapo ulipo?, Baada ya kupata majibu hebu iambie nafsi yako kwamba atabadilika na amini ameshajifunza kwa makosa na kisha msamehe kabisa, kwa hatua hii utakayochukua ndiyo ambayo itakufanya uweze kuona wepesi nakujikita katika mambo yako yatayokufanya upige hatua katika mafanikio. Ukisoma Biblia utaona ata Yesu mwenyewe walimkosea na kumtesa sana lakini mwisho wake aliinua kichwa chake juu na kusema Baba wasamehe maana hawajui walitendalo. hadi hapo unakuja kuona kwamba binadamu anafanya kitu pasipo kufahamu kwa maana hajakamilika hivo yatupasa tusameheane ili tuelekeze nguvu kubwa katika kusaka mafanikio na sio nguvu katika kulipiza visasi.
Pasipo kupoteza maana ya somo hili nieleze sasa ni kwa nini ni muhimu kusamehe;-
1. Huongeza furaha ya moyo(piece of mind)
Kusamehe mtu mwingine humfanya mtu huyo kuwa huru kwa kila jambo ambalo analifanya. Kwani kama nilivyosema hapo awali ya kwamba watu wengi tumebeba mizigo mizito ndani ya nafsi zetu, hata hivyo kutoka na mizigo hiyo mizito tunashindwa kupiga hatua za kimafanikio. Hivyo ili kuweza kupiga hatua za kimafanikio hatuna budi kuweza kujifunza kuweza kuwaaemehe watu wengine waliowahi kutokosea . Hata vitabu vya dini vinatukumbusha ya kwamba Mungu tabia yake kusamehe hivyo nasi hatuna budi kusamehe wengine. Vitabu hivyo hivyo vya dini vinasema ya kwamba saba Mara sabini. Na endapo utasamehe unafungua milango ya mafanikio yako.
2. Kusamehe ni njia ya mafanikio.
Endapo leo utaamua kusamehe ni ishara ya kwamba utaondokana katika sakata la kuwa katika wimbi la mawazo , hata hivyo kupelekea wewe kuwa na mawazo chanya, mara kadhaa watu ambao hawana ule moyo wa msamaha kwa namna moja ama nyingine huwa hawapo sawa kwani huwa hawa amani hata kidogo, hata hivyo kama kweli uyataka Maisha yawe sawa ni muda wako sahihi wa kuvutua vile vyote vilivyomo katika nafsi yako kinyume cha hapo utakuwa unapotea hajalishi ulikwazika kwa kiasi gani. Pia ukumbuke wabaya watu, pia watu hao hao ndio wazuri na wana mchango mkubwa katika safari yako ya mafanikio.
3. Kusamehe huimarisha afya.
Afya njema ni njia ya kupata Mafanikio, moja ya kanuni ya kutaka kupata Mafanikio ni kwamba unahitaji kuwa na afya njema ili uweze kuimarika na kupata Mafanikio hayo. Hebu tutafakari kidogo hivi leo ukipata ugonjwa wowote na kukufanya usiweze kuendelea na kazi yako hivi huwa unaathirika kwa kiasi gani katika jambo lako? Kama umepata majibu Nafikiri utakuwa umeona umuhimu wa kuwa na afya njema.
Hivo mpendwa rafiki hebu chukua nafasi leo kuwasamehe wale wote waliokukosea na ujikite katika kutafuta mafanikio, na kuanzia leo amini hakuna mtu mkamilifu ata wewe umewakosea wengi ka kujua ama kwa kutokujua kukosea kupo tu hivo yatupasa tusameheane. nikutakie siku njema na utekelezaji mwema wa kusamehe waliokukosea.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email :fanuelmwasyeba@gmail.com