habari ya leo rafiki yangu ni siku nyingine tena tunakutana hapa hapa kwenye kijiwe cha maarifa chanya ya mafanikio,lengo au adhma yetu ni kumuona kila mmoja wetu amefanikiwa. Mpendwa rafiki kama tusemavyo kila siku mafanikio sio miujiza kwamba inatokea tu hapana mafanikio ni mipango na muendelezo wa mikakati unayotenda katika maisha yako ya kila siku, mafanikio ni tabia najua hapo utajiuliza mafanikio ni tabia kivipi, mpendwa rafiki acha nikuambie watu wote waliofanikiwa wana tabia tofauti na watu wengine na ndio maana wamefanikiwa. Zipo tabia za mtu mwenye mafanikio ambazo mpendwa rafiki ukijifunza na kutendea kazi ni lazima ufanikiwe. .afanikio yanahitaji kukana nafsi yako na kuachana na vitu vya mazoea ambavyo kila mtu anafanya na kujikuta uko pale pale kila siku unahitaji kubadilika na kuamua kuiga tabia za wana mafanikio ili upate mafanikio.
Leo twende tuangalie tabia za mtu aliyefanikiwa au anaetaka kufanikiwa aweje,mafanikio yana hatua zake na sheria zake ambazo kwa mtu yeyote atakaefuata ni lazima apate mafanikio, zifuatazo ni tabia saba za mwana mafanikio:-
1.anajizungumzia Vema ( anajiamini), mwanamafanikio anajiongelea vema,hajikatishi tamaa daima anasonga mbele huku moyoni mwake akijiambia nitafanikiwa tu, mwana mafanikio mdomoni mwake na moyoni mwake ana neno mafanikio basi haofii kushindwa bali huamini kama ni changamoto inayompeleka katika mafanikio makubwa, hivo mpendwa rafiki ukitaka kupata mafanikio anza kujitamkia ushindi wewe mwenyewe na kuamini utafanikiwa.
2.ana maono chanya na ameyaandika ,mwanamafanikio muda wote anatazama malengo yake yatakamilika vipi na kuandaa mikakati ya kufikia malengo hayo, hakuna mafanikio bila maono maono ndiyo dira pekee inayokupeleka kwenye mafanikio, kila aliyefanikiwa alikuwa na maono na kuyaandika na kuanza kufanyia kazi, kama unataka kufanikiwa anza kuwa na maono na hakikisha unayaandika na kila siku yapitie na kuyatekeleza utafanikiwa.
3.Amezungukwa na watu chanya,mwanamafaniko anapenda marafiki na watu wenye matokeo chanya ili ajifunze kutoka kwao, mwana mafanikio amechagua watu waliomzunguka kwa maana ukizungukwa na watu wenye mitazamo hasi basi na wewe utakuwa na mtazamo hasi, ila ukizungukwa na watu wenye mtazamo chanya basi na wewe utakuwa na mtazamo chanya, sasa ukitaka kufanikiwa kwanza tazama ni watu gani wamekuzunguka kama hawana faida yoyote kwako anza kuwaepuka na ungana na watu waliofanikiwa ili ujifunze na kuhamasika kutoka kwao.
4.Anakula chakula chanya cha ubongo(positive mental food).mwanamafanikio kila siku lazima ajifunze kitu kipya ili kupata mbinu na maarifa mapya,anajifunza kutoka kwenye audio book,educational,insparational and motivational To know something new, ubongo wa mwanadamu kila siku unahitaji kitu kipya ili uweze kukua sasa wana mafanikio wanapenda kutumia muda wao mwingi kujifunza jambo jipya kutokana na kile anachokifanya, mpendwa rafiki kama unataka kufanikiwa anza kujifunza jambo jipya kila siku kutokana na kile unachokifanya mfano kama unafanya biashara anza kujifunza kitu kipya kila siku ili kuboresha biashara yako basi hapo utafanikiwa, anza kujifunza kutoka katika vitabu mbalimbali vya mafanikio, mitandao mbalimbali kama huu Rise Africa na mingineyo.
5.fikiria maendeleo chanya(Think positive development).nia ya mwanamafanikio ni kupata maendeleo chanya,hivo ufanya kazi kwa bidii ili apate maendeleo chanya, lengo kubwa la mwana mafanikio ni kupata mafanikio na maendeleo katika kutimiza malengo yake hivo afanyi uzembe wala kupoteza muda kwani ana amini kufanya hivo ni kupoteza fursa ya kimaendeleo hivo ufanya kazi kwa bidii na kujituma hivo wanapata mafanikio, basi kama mpendwa rafiki unataka kuwa mwana mafanikio anza kufikiri maendeleo chanya katika kile unachofanya.
6.Afya bora,mwanamafanikio anazingatia sana afya bora,anahakikisha anafanya mazoezi, anakula chakula bora,analala mapema,anaamka mapema, ana amini sana afya yake kwamba ndiyo mtaji bila afya hakuna maendeleo hivyo huilinda afya yake kwa umakini mkubwa, mpendwa rafiki kama upo miongoni mwa wanaotaka mafanikio anza kuilinda afya yako kwa maana afya yako ikiteteleka basi hakuna chochote utakachofanya au kutimiza ata kama ulikuwa una maono mazuri kiasi gani, hivyo fanya mazoezi, kula vizuri, lala mapema, amka mapema utafanikiwa.
7.Anajari sana muda wake, katika kitu ambacho mwana mafanikio hapendi ni kupoteza muda wake mwingi katika mambo ambayo hayana faida hivo ana amini kwamba muda ukipita haurudi tena hivo anapopata nafasi basi huitumia kwa usahihi na ubunifu zaidi ili kupata mafanikio, hivyo mpendwa rafiki kama unataka mafanikio anza kujari muda kataa mtu kuupoteza muda wako bila sababu ya msingi jifunze kusema hapana utafanikiwa.
Mpendwa rafiki tembea katika tabia hizi naamini maisha yako hayatakuwa kama ulivo leo,asanteni sana nakutakia siku njema.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email :fanuelmwasyeba@gmail.com