MAKALA: HUU NDIO UONGO UNAOJIDANGANYA MWENYEWE NA KUSHINDWA KUFANIKIWA


Jaza fomu hii kupata masomo yetu kwa njia ya email

* indicates required


Habari za muda na wakati huu mpendwa rafiki wa mtandao wetu wa Rise Africa, ni matumaini yangu u mzima wa afya.Napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha katika makala zetu ambapo tunashirikishana mambo mbalimbali yahusuyo mafanikio.
Mpendwa rafiki leo nakukaribisha tushirikishane na kuona uongo ambao watu wengi hujiambia na kujizuia kufanikiwa, mpendwa rafiki kila mtu ukimuuliza kwanini hajafanikiwa basi atakupa sababu kibao, mfano ukimpa mtaji afanye biashara atakuambia mtaji ni mdogo, akianzisha biashara haisimamii vema ikianguka utasikia anasema wateja hakuna, mala uchumi mbaya, yaani hakosi sababu.
Mtu pekee anaezuia mafanikio yako ni wewe mwenyewe, sio jamii yako, sio serikali, wala sio mtu yeyote katika maisha yako. Naamini kwamba hakuna mtu aliyezaliwa akiwa bora kuliko mwingine, lakini naamini kuwa kila mmoja ana uwezo wa kupata mafanikio.
      Haya twende tuangalie sababu 4 za `uongo zinazosemwa na watu kila muda zinazowafanya washindwe kufanikiwa:-
1 Nahitaji shahada ili niweze kufanikiwa.
Huu ni uongo unaosemwa mala nyingi na watu wengi ambao wameshindwa au kushindwa kufanikisha malengo yao. mpendwa rafiki mafanikio hayahitaji kisomo kikubwa bali ni uamuzi wako toka moyoni ni kwa namna gani unahitaji kufanikiwa na kuweka jitihada kubwa katika kile unachokiamini. ukitazama mbona kuna watu wamepata shahada lakini bado hawajapata mafanikio. ukiwa mjasiriamali unakuwa boss wa biashara yako mwenyewe, hutaji elimu ya chuo kuanzisha biashara na huitaji shahada kujifunza juu ya kile unachotarajia kufanya. Kuna mifano mingi ya watu waliofanikiwa waliotengeneza mafanikio yao bila kuwa na shahada mfano mwanzirishi na mmiliki wa mtandao wa facebook Mark Zuckerberg.
2 Sina muda wa kutosha.
Hii ni sababu kubwa ya uongo ninayoisikia kila siku, mpendwa rafiki hakuna mwanadamu ambaye muda unamtosha, muda hautoshi kufanya kila kitu bali muda unatosha kufanya kitu cha muhimu, kama una muda wa kuperuzi mitandao ya kijamii au kucheza game basi jua una muda wa kutosha, acha kupoteza muda anza kufanya mambo yatayokupa mafanikio.
siku zote watu ni wavivu wanashindwa kuamka mapema au kutumia muda mwingi kufanya mambo yanayokuletea mafanikio, una muda mchache sana kuliko mtu mwingine mtu mwingine ila tambua kufanya kitu ata kidogo kila siku tena kwa bidii amini utaendelea na kufanikiwa kuliko yule aliyekaa tu anza sasa muda unao.
3 umri umeenda
Ili pia limekuwa ni sababu ya watu wengi ambayo wanasema imewazuia kufanikiwa, watu wengi ukiwaambia wafanye jambo fulani la mafanikio wanadai umri umeenda, mpendwa rafiki kama unauwezo wa kufikiri basi una umri wa kufanya kazi na kufanikiwa, haijalishi umri wako ni miaka mingapi, bado umri haujaenda usikate tamaa anza sasa weka juhudi katika kile unachofanya utafanikiwa, mfano mmiliki wa migahawa ya KFC Colonel Harland sanders alifanikiwa na kuwa billionea akiwa na miaka 88, bado hujachelewa mafanikio hayana umri inuka na anza utafanikiwa.
4 Ni vigumu kuanza
Huu pia umekuwa msemo wa watu wengi, watu wengi wanasema wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wanashindwa waanze vipi, mwingine anasema ana mtaji kabisa lakini inamuwia vigumu aanze kufanya kitu gani, au aanze vipi kufanya biashara, mpendwa rafiki hakuna mafunzo yanayofundisha kuanza kitu, wewe mwenyewe ndio mwenye maamuzi ya kuanza, anza sasa kama unataka kuanza. Napoleon anasema " kuna ugumu katika kuanzisha safari lakini pale unapoanzisha tu basi safari huanza", anza kuchukua hatua na pindi utapochukua hatua utashangaa unavyoendelea na kufanikiwa.

Inasikitisha kuona watu wengi hawafanikiwi kwa sababu ya uongo wanaojiambia wenyewe. Napenda kukuambia mpendwa rafiki kama bado upo hai basi una nafasi ya kufanikiwa, maamuzi yako mikononi mwako wewe ndiyo wa kuamua nini kifanyike katika maisha yako, kikwako pekee kinachokufanya usifanikiwe ni wewe mwenyewe. Chukua hatua sasa badilika. nikutakie siku njema mpendwa rafiki.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email            :fanuelmwasyeba@gmail.com