MAKALA: HUU NDIO UGONJWA HATARI KWA MAFANIKIO

Habari za jumapili mpendwa rafiki wa mtandao wetu wa Rise Africa, ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya. Karibu kwa mala nyingine tushirikishane mambo mbalimbali yahusuyo mafanikio, katika makala ya leo tunaenda kuangalia ugonjwa hatari na mbaya kwa mafanikio.
  Mpendwa rafiki ugonjwa huu ni hatari, ni ugonjwa ambao unakandamiza mafanikio yako na kujikuta unabaki vilevile kila siku, ugonjwa, ugonjwa huu unaitwa kughairisha au kuhairisha.
 Maana ya ugonjwa huu ni "kuwa na tabia ya kughairi au kuahirisha mambo maram kwa mara " ugonjwa huu ni adui mkubwa wa mafanikio.Watu waliofanikiwa kamwe hawalalamiki ,hawaongei sana .Kamwe hawaarishi jambo walilopanga walifanye au wasilifanye ,lakini hawakwamishi kuendelea kufanya jambo .Lakini watu wadhaifu hupenda kuahirisha mambo .Kupona ugonjwa huu mpendwa rafiki dawa ni moja tu.
Acha lugha dhaifu kutoka katika matamshi yako,kataa kabisa kusema lugha dhaifu au maneno ya kukata tamaa kama"Nitajaribu"au "Nitafanya tu".Haya ni maelezo ya kughairi jambo kulifanya kwa ufanisi.Pindi mtu mmja anaposema "Nitajaribu kufanya baadaye",kusema hivi wanamanisha "Nakupa ishara kabisa kabisa kwamba naenda kushindwa kufanya".Siendi kufanya jambo hilo kwa wakati,usinilaumu kama sijamaliza kazi. 
    Mpendwa rafiki wapenda kughairi mambo kama kufanya ujihisi mdogo na dhaifu.Kila anajua kwamba wapenda kughairi mambo siyo watu makini na ni watu tegemezi katika kila hali.Nakutakia siku njema mpendwa rafiki.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email            :fanuelmwasyeba@gmail.com