DIRA YETU: MAFANIKIO SIO AJARI

Habari za leo mpendwa msomaji wa makala zetu za rise africa naamini kila siku unajifunza kitu kupitia mtandao wetu na natumaini unapiga hatua kila siku kufikia mafanikio, leo tunaenda kushirikishana dira yetu kama wana familia wa mtandao wa rise africa karibu.
Dira yetu tunaamini kwamba mafanikio sio ajari bali ni mikakati na mipango ambayo mtu anapanga kufikia mafanikio, unajua watu wengi au mitaani kwetu utasikia msemo " leo kwangu kesho kwangu" au utasikia " aliyekupa wewe ndiye kaninyima mimi", mpendwa rafiki naamini misemo hii unaijua vizuri na umeisikia mala nyingi, mimi napenda kukuambia leo kwamba misemo hii haina uhalisia wowote wala ukweli kwa sababu, Mungu hakumuumba mtu mwingine kumpa mafanikio na mwingine kumyima hapana sote alituumba kwa usawa hakumpa mtu utajiri wala umasikini bali alitupa ufahamu kwahiyo vile unavyofikiri ndivyo utakavyo kuwa.
wakati najaribu kulitafakari hili nilipeleka mawazo yangu wakati tukiwa watoto watu wote tulikuwa sawa na tumecheza pamoja sasa kwanini tunakuja kutofautiana kimafanikio?, hapo nikapata jibu kwamba kwa namna mtu anavyofikiri kila siku ndivyo atakavyokuwa, ukifikiria mambo hasi basi umechagua kuwa masikini na ukifikiri mambo chanya basi utafanikiwa. Hivo kufanikiwa au kutokufanikiwa kupo mikononi mwetu sisi wenyewe.
Mpendwa rafiki mafanikio sio muujiza, wala sio kitu kinachokuja tu, kila kitu kinatokea kwa sababu iwe nzuri au mbaya, hasi au chanya, kwa namna unavyopangilia vema kuhusu kile unacghotaka inakulazimu ujifunze kwa wale waliofanikiwa katika jambo hilo kabla yako, na ukatendea kazi utapata matokeo sawa na waliyoyapata wao.
Tukiangalia Biblia inasema "kimjaacho mtu ndicho kimtokacho",hivyo huwezi kuonyesha kitu ambacho hudi hapa tunaona "kila kitu kinachotokea kwa sababu ;na kwa kila matokeo kuna sababu yake"Aristotle anasema tunaishi katika ulimwengu unaotawaliwa  na sheria na nafasi endelevu kusema kila kitu kinatokea kwa sababu yake kwa kujua au kutokujua sababu hiyo na kusema kila tokeo lina sababu yake.
Hivyo kitu muhimu hapa ni kwamba fikra zetu ndiyo sababu na hali zetu ndiyo matokeo, hivyo vile tunavyofikiri ndivyo tulivyo, Hivyo mpendwa msomaji Mafanikio sio ajari wala hayaji kama muujiza bali ni mipango kuna msumo unasema " ukishindwa kupanga basi umepanga kushindwa", hivo tuishi na tuenende katika mikakati na utekelezaji kwa nidhamu tutafanikiwa, lakini tukisubili mafanikio yaje kama ajali mpendwa rafiki napenda kukuambia kamwe hutokuja kuyaona. hivo wito wangu ni tuishi kwa malengo tutafanikiwa. nakutakia siku njema mpendwa rafiki.
Mwandishi: Mwasyeba Fanuel
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email            :fanuelmwasyeba@gmail.com

Related Posts