Habariza muda na wakati kama huu mpendwa msomaji wa makala yetu, ni matumaini yangu u mzima wa afya, asante kwa kuwa nasi bega kwa bega katika kushirikishana, kujifunza na kupambanua siri za kufanikiwa na utumie mbinu gani kufanikiwa. Kuna rafiki nilikutana nae akaniambia kuwa yeye ana mipango na malengo makubwa ila tatizo anashindwa kufanikisha sababu kila akitaka kuanza basi mambo mengine yanajitokeza, najua watu wengi tuna mikakati ya kutufanya tufanikiwe lakini tatizo linakuja tunashindwa kuikamilisha mikakati hiyo na inabaki kama ndoto tu, wengine tumezongwa na mambo mengi mpaka tunashindwa kukamilisha mambo yetu muhimu na kujikuta kila siku tuko pale pale, basi leo mpendwa rafiki napenda nikushirikishe kanuni ya ABCDE katika kufanya shughuri zako za kila siku, ukiitumia vema kanuni hii utaweza kufanya mambo yako kwa mikakati na kupata mafanikio makubwa.
Kwa namna unavyowekeza katika kupanga na kuandaa vipaumbele kabla hujaanza, ndivyo vitu vingi muhimu utafanya na utamaliza haraka baada ya kuanza. Watu wengi tunaingia kwenye jambo fulani kabla ya kufanya utafiti juu ya jambo hilo, hivo kujikuta tunaingiliwa na kupata hasara kubwa , mfano watu wengi wanaingia kwenye biashara bila kuchunguza hivo wengi wanaishia kupata hasara. hivo kabla hujaanza jambo lolote anza na mipango kabla hujaingia kulifanyia kazi jambo hilo utafanikiwa.

Kanuni ya ABCDE ni njia nzuri katika kupangilia mambo yako muhimu utakayokwenda kuyafanya kila siku. Mbinu hii ni rahisi na ni nzuri itakayokufanya ufanye mambo yako vizuri na kwa ufanisi mkubwa.Nguvu ya kanuni hii ni rahisi sana na hapa tutaenda kuona inafanyaje kazi.
Kwanza anza na kuoroghesha mambo unayoyafanya au unayoenda kuyafanya kwa siku inayofuata, orodhesha kwenye daftari yako ya malengo kisha weka A, B, C, D, na Ekatika kila jambo kwenye orodha yako kabla hujaanza kufanya kitu chochote.
A-Ni jambo ambalo ni muhimu sana, jambo hili ni lazima ulifanye hili ni jambo ambalo linaleta matokeo makubwa endapo utalifanya au kutokulifanya, mfano kwa mwanafunzi jambo A ni kusoma hivo akisoma atafauru asiposoma atafeli hvo jambo A ni muhimu sana. kama kuna jambo muhimu zaidi ya moja unaorodhesha kwa kuipa herufi A-1, A-2, A-3 na kadharika katika kila kitu zingatia A-1 hilo ndilo jambo muhimu sana kuliko yote.
B-Hili ni jambo ambalo utalifanya lakini lina matokeo ya kawaida, hii tunaweza kuiita kazi ya ziada katika maisha yetu. Hii ina maana kwamba ni kazi ambayo inamfanya mtu kukosa furaha kama asipofanya lakini sio muhimu kama jambo A mfano kuchat, kuingia katika mitandao ya kijamii na kadharika hii inaweza kuwa jambo B. kanuni inasema hivi kamwe usifanye jambo B kama jambo A bado hujalifanya. Usichanganywe na jambo B kama bado kuna jambo muhimu bado hujalifanya.
C-Hili ni jambo ambalo ni zuri kulifanya lakini halina maendeleo yoyote yale endapo utalifanya au kutokulifanya. Jambo C linahusisha kupigia simu marafiki, kutazama habari au mechi, kuongea na marafiki na kadharika, yaani ni kazi ambayo matokeo kabisa na marafiki kabisa katika maisha yako.
D-Hili ni jambo unalifanya kwa kujitolea kwa wengine, kanuni inasema unatakiwa kujitolea kila kitu ambacho kila mtu anaweza akafanya, ili uwe huru na kupata muda mwingi na jambo A ambalo ni wewe pekee unawezaukafanya.
E-Hili ni jambo ambalo unaweza uukaliacha ata kama linaweza kuleta utofauti katika maisha yetu, hili linaweza kuwa ni jambo muhimu kwa muda lakini sio uhalisia sana katika maisha yetu hii inaweza kuwa jambo unaloweza kufanya nje na mwenendo wako au kwa sababu unapenda furahia kufanya jambo hilo.
Baada ya kuifanyia kazi kanuni ya ABCDE kwenye orodha yako sasa kwa pamoja unganisha na kuwa tayari kufanya mambo muhimu kwa haraka sana. ili kuifanya kanuni hii ya ABCDE ifanye kazi kwako kitu cha msingi ni kuwa na nidhamu binafsi kuanza mara moja kwenye A-1 fanya hiyo mpaka utapomaliza . Fanya jambo moja likiisha ndipo uingie lingine.
Nashukuru kuwa pamoja nami naamini umejifunza kitu katika kupiga hatua kufikia matokeo makubwa, nakutakia siku njema na kila siku jitahidi kuwa bora zaidi kuliko jana.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano:0717262705/0683636572
Email: fanuelmwasyba@gmail.com