TOKA CHINI KWENDA JUU: SHERIA YA MAISHA

Habari za leo mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa mtandao wa Rise Africa, ni matumaini yangu u mzima, nakukaribisha tena twende tukajifunze kanuni mbalimbali ambazo zitatuwezesha kutimiza malengo yetu makubwa katika maisha. Rafiki katika maisha kila mwanadamu ana mipango yake lakini tatizo lipo katika kuitimiza mipango hiyo na hapa ndipo linapokuja swali la kwanini watu wengine wanafanikiwa na wengine wanashindwa kufanikiwa, twende tuungane pamoja kujifunza kanuni hizi zitakazo kutoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Maisha ni jumla ya kila kitu akifanyacho mwanadamu, katika maisha mwanadamu amelenga kupiga hatua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, kila mwanadamu anatarajia maisha mazuri na yenye mafanikio lakini cha kushangaza kunakuja kutokea watu waliofanikiwa na watu wasiofanikiwa. Kuitazama sheria ya maisha tuanze na swali hili "kwanini baadhi ya watu na makampuni wanafanikiwa zaidi kuliko wengine?", kitu kikubwa nilichoanza kujifunza kutoka katika sheria ya Aristotle ya usababishi (principle of causality), siku hizi inaitwa sheria ya sababu na matokeo (The law of cause and effects).
   1 SHERIA YA SABABU NA MATOKEO ( THE LAW OF CAUSE AND EFFECT)
Mpendwa rafiki hapa duniani kila kitu kimetokea kwa sababu fulani, kwa kila matokeo kuna sababu yake maalumu. Rafiki sheria hii inasema kwamba mafanikio, utajiri, furaha, biasharani matokeo ya chanzo au sababu fulani.
Rafiki ukiitazama bahari na uwingi wake wa maji chanzo cha maji yote yale ni mito, hivo hakuna chochote kinachokuwepo duniani bila ya sababu, hapa tunaona kwamba kama utakuwa na sababu chanya na mikakati thabiti utapata matokeo chanya. katika kujuifunza zaidi kanuni hii tuitazame kwa undani zaidi:-
           *Mafanikio sio ajari
Mpendwa rafiki mafanikio sio ajari na wala sio muujiza wala sio kitu kinachotokea tu kama zari, Kila jambo linatokea kwa sababu fulani iwe nzuri au mbaya, hasi au chanya.
- Sir Isaac Newton anaitaja katika sheria ya tatu ya mwendo(third principle of motion) state that "for every action, there is an equal and opposite reaction", kwetu sisi fikra ni sababu na hali ni matokeo, hivo kuwa na fikra chanya ili upate matokeo chanya.
          *fikra ni ubunifu
Rafiki fikra zako ndio ubunifu wako wa kwanza unaosukuma maisha yako, unaweza ukaunda dunia uitakayo kwa namna utakavofikiri.
- Pindi utakapobadilisha fikra zako utabadili na maisha yako, sheria bora katika mafanikio ya mtu na biashara kwa ujumla ni " utakuwa kama unavofikiri mara nyingi".
Ralph waldo Emerson aliandika kwamba "kila kampuni kubwa nyuma yake kuna nguvu ya mtu mmoja".
            * Chaguo lako ndio maisha yako
Mpendwa rafiki siku zote uko huru kuchagua kila ukitakacho, hakuna mtu wa kukusukuma uchague au kufikiri, vile ulivyo ni matokeo ya namna unavyoishi na unavyofanya, kila siku fira na mawazo ya binadamu yanabadilika, na yanaathiri maisha yako, hivo fanya uchaguzi sahihi chagua kujituma na kuweka bidii katika kazi na utafanikiwa.

sasa twende tuangalie ni kwa namna gani unaweza kuitumia hii sheria katika maisha yako:-
- Chambua sehemu mbalimbali muhimu katika maisha yako na kisha tazama uhusiano kati ya sababu na matokeo ya vile unavyofikiri.
- Kuwa mkweli kwa nafsi yako tazama uhusiano wa unavyofikiri juu ya maisha yako na namna unavyoishi.

Natumaini umejifunza kitu mpendwa msomaji, chukua hatua leo angalia kila kitu ukifanyacho tambua kuna matokeo yake, kuna usemi usemao utavuma ulichokipanda, panda fikra chanya na mipango thabiti na utapata matokeo bora. Ila siku zote nasema uchaguzi ni wako kufanikiwa au kutofanikiwa ni maamuzi yako, wewe ndie kiongozi wa maisha yako hakuna mtu atakaekuja kukusimamia katika maamuzi yako hivo fanya uchaguzi sahihi.

Mwandishi; Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano; 0717262705/0683636572
Email         ;     fanuelmwasyeba@gmail.com