Habari mpendwa rafiki na mfuatiliaji wa mtandao wetu wa Rise Africa, tumekuwa pamoja katika kuhamasishana na kupeana mbinu mbalimbali za kufikia mafanikio, ni imani yangu kuwa kila siku unazidi kubadilika na kuwa mtu wa kupiga hatua kila siku kuelekea mafanikio makubwa. K ama bado upo pale pale nakupa pole na hakuna namna ya kukubadilisha, kila siku nasema wewe mwenywe ndiye mwenye maamuzi ya kuchagua kufanikiwa au kutokuyfanikiwa, hakuna mtu atakaeweza kukushika mkono kukuvuta kuelekea mafanikio, hivo kuwa maskini au kuwa tajiri ni maamuzi yako binafsi.
Mpendwa rafiki nakukaribisha katika segmenti mpya iitwayo TOKA CHINI KWENDA JUU, hii ni segmenti mpya tutakayoianza 24/7/2017, segmenti hii inahusisha sheria mbalimbali za kufanikiwa katika biashara, ili ufanikiwe katika biashara unahitaji kanuni zitakazokuongoza kufanikiwa katika biashara yako. ni furaha yangu kukukaribisha kufuatana pamoja nami kuzitazama kanuni hizi na kuchukua hatua kuzifuatanaamini biashara yako haitabaki kama ilivyo.
nikutakie usiku mwema na maandalizi mapya ya siku mpya ya kesho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)