habari za muda na wakati kama huu rafiki yangu, kila siku tunazidi kushirikishana mambo muhimu yatayotufanya tufanikiwe katika maisha yetu, binadamu ameumbwa ana hasira ndio maana unaweza kukuta mtu akichukizwa anaweza ata akamuua mwenzake yote hayo ni kwa sababu ya hasira, hili ndo limetuleta kwenye makala ya leo ambayo tutaangalia ni jinsi gani uitumie hasira yako kuchukia udhaifu wako karibu.
Mpendwa rafiki kila mtu duniani ana udhaifu asikudanganye mtu kuwa yeye hana udhaifu Kama wewe ni binadamu basi lazima una udhaifu,cha msingi na muhimu tambua udhaifu wako,hebu jitathmini nini udhaifu wako unaokukwamisha kufikia malengo yako,kuna udhaifu wa aina nyingi kwa mfano kukosa ujasiri, usingizi, uvivu, uzembe, kukosa uvumilivu, hofu nk,katika kushinda udhaifu unapaswa kukuza akili yako kujua kile unachokiamini, uilazimishe ifanye kile unachotaka.
sasa ile hasira unayoitumia kutaka kupigana itumie kuchukia udhaifu wako ambao unakufanya mpaka leo usipige hatua yoyote ya kimafanikio, watu wote waliofanikiwa waliamua kutumia hasira zao kuukataa udhaifu wao na kuchukua hatua na kujifunza sana na hii ikawafanya wafanikiwe, hivo kama unataka kufanikiwa ni lazima uchukie na kukataa udhaifu wako.
Sasa hebu tuangalie ni kwa namna gani tunaweza kutumia hasira zetu kuchukia udhaifu wako:-
Anza kujitambua mwenyewe
Mpendwa msomaji tumia hasira yako kujitambua wewe mwenyewe katika maeneo yote ya maisha yako, weka nguvu kubwa katika kujitambua, jitambue wewe ni nani, upo hapo ulipo kwa sababu gani, kwanini upo hivo ulivo mpaka leo, katika kutambua haya utajua udhaifu wako ni nini na ukachukua hatua kuukataa na kuchukua hatua mpya ya kimafanikio, mfano mtu hajari muda na kumfanya akose mafanikio
Nyamazisha akili yako.
Watu waliofanikiwa walitumia nguvu kubwa kunyamazisha akili zao kuwaza au kuogopa mambo yasiyo ya msingi na kujikita katika mambo muhimu yanayowaletea mafanikio, hivo basi tumia hasira yako kuinyamazisha akili yako ikatae udhaifu wako na jipe ujasiri kwamba na wewe unaweza kufanya mambo makubwa.
Tambua thamani yako.
Udhaifu wako ndio uliokufanya uikose thamani yako mpaka leo, hofu yako ya kufanya mambo ndio uliokufanya mpaka leo uwe hapo ulipo, hivo basi tumia hasira yako kutambua thamani yako, kugundua thamani yako jiulize ni vitu unapenda kufanya na ukifanya vinakupa furaha, mfano mtu anapenda kufanya biashara lakini ana hofu, sasa jiulize ni kwanini unakuwa na hofu, baada ya kujua udhaifu wako changanua mbinu unazotumia kufanikisha kazi yako kwa furaha na ujasiri kitu ambacho kitakupa thamani yako.
Jitaarifu mwenyewe
Mpendwa msomaji kitu muhimu katika kuukataa udhaifu wako ni kujitaarifu mwenyewe kwamba huutaki tena udhaifu wako, jipe ahadi na ujasiri mkubwa kwa kuchukua hatua, fanya kile ulichokuwa unakiogopa wewe kifanye na utaona matokeo makubwa, mfano kama unashindwa kuamka asubuhi na mapema anza kuweka alarm na jiambie mwenyewe ikifika muda huo lazima uamke hivo ukiweza siku ya kwanza basi ni hatua bora ya kuuacha udhaifu wako, hebu jiambie mwenyewe kwamba unaweza na wewe ni bora kuliko mwingine hii itakutia hamasa ya kukupa nguvu na mbinu nyingine ya kuepuka udhaifu wa kufanya kile ulichokuwa unashindwa kufanya.
Soma vitabu kuhusu kitu unachokihofia
Mbinu nyingine ya kuepuka udhaifu wako ni kusoma zaidi vitabu mbalimbali mfano unataka kuingia kwenye biashara anza kwanza kupata elimu ya biashara ifahamu vema hii itakufanya uondokane na udhahifu wako na kuingia kwenye biashara kwa ujasiri mkubwa. Kusoma vitabu kunakupa hamasa ya kukijua kitu kwa undani na kuona mifano ya watu mbali mbali ambao wamefanikiwa kwenye hicho kitu unachotaka kukifanya.
Mpendwa rafiki udhifu ni kikwazo kikubwa katika safari ya mafanikio hivo tumia hasira uliyo nayo kuuchukia na kuukataa udhaifu wako ili kupata mafanikio, nakutakia siku njema
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email: fanuelmwasyeba@gmail.com