MAKALA:KWANINI WATU WALIO FANIKIWA SANA WANA MAADUI WENGI

habari za asubuhi mpendwa rafiki yangu ni jambo la kumshukuru kukutana tena hapa hapa katika kijiwe cha mafanikio karibu,katika mafanikio yetu tunahitaji maadui zaidi kuliko marafiki,najua utashangaa na kujiuliza kuwa hatuitaji marafiki??, no marafiki ni wazuri sana na muhimu,rafiki anakupa company lakini adui anakupa promotion,watu wasio wa kawaida katika eneo lolote lazima utachukiwa na watu wa kawaida.
   Ukisoma biblia Daudi alimuhitaji Goriati ili awe mfalme,Yesu alihitaji maadui wa kumuua ili kazi yake ya ukombozi ikamilike, hivo tunapaswa kusoma mambo mengi kupitia adui na adui ni kama ngazi yetu katika mafanikio, hakuna mtu ambaye amefanikiwa hana maadui hii inakuja kwa sababu wengine wanakuchukia kwa sababu umewazidi, wengine wivu, wengine wanakuchukia bila sababu na wengine kibao.
    Tukimrejea mwandishi Robert Greene katika kitabu chake cha 48 laws of power anatupa sheria moja ya kufanikiwa ni "never put too much trust to friends, learn how to use enemies",yaani kamwe usimuamini sana rafiki ila jifunze kuwatumia maadui, Watu wengi waliofanikiwa wanasema kwamba kama unataka mafanikio makubwa, unatakiwa uwe tayari kuwa na maadui na kuchukiwa, maadui ni watu wanaofikiri wanajua misingi ya mafanikio, lakini hata siku moja hawajawahi kuchukua hatua kufika huko, hivo kukuona wewe umefika huko basi ndipo chuki uanzia hapo.
Kama ukitaka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio unatakiwa kutafuta njia ya kuwasoma maadui zako na kila chuki zinazokuja juu yako, njia ya kubadili wanavyokupinga, chuki, wivu wao kuwa mafuta unayotumia kuendeshea gari ya mafanikio, unahitaji chuki zao zaidi kwa maana katika chuki hizo kuna fursa ambayo utaitumia kufanikiwa. Hivo ukiona unazidi kuwa na maadui wengi jua ndio unavozidi kufanikiwa.
nakutakia asubuhi njema 
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email:           fanuelmwasyeba@gmail.com

1 comments: