UKITAKA KUFANIKIWA ANZA NA KUUTAWALA MUDA

Muda ndio funguo kuu ya mafanikio ukiweza kuutumia muda wako vizuri basi kufanikiwa kwako ni lazima na ukishindwa kuutumia muda wako vizuri basi sahau swala l;a kufanikiwa, mpendwa msomaji sisi waafrika tupo nyuma sana katika matumizi ya muda, tunatumia muda mwingi katika mambo yasiyo na faida kwetu, mfano tunapoteza muda mwingi katika kusalimiana utakuta watu wanasalimiana masaa mawili huku ni kupoteza muda. wanadamu hatuko sawa katika kila kitu lakini Mungu alitupa kitu kimoja ambacho ni sawa ambacho ni muda, wanadamu wote tumepewa masaa 24 na katika masaa hayo hayo kuna walio fanikiwa na wengine kushindwa kufanikiwa. Leo napenda tujifunze namna gani tutumie muda wetu kwa kupata mafanikio twende pamoja.
Kuutawala muda ni uwezo wa kuutumia muda vizuri na kwa faida, kuna msemo unaosema muda ni pesa, ukiutazama msemo huu utagundua kwamba kwa namna unavotumia muda wako ndivyo unavoweza kutengeneza pesa, kuna vikwazo mbali mbali vinavyotufanya tushindwe kuutunza muda wetu kama vile mtu kutokujali jinsi ya kuitumia dakika moja, kupenda kuhairisha mambo, kupenda kurudia rudia jambo, kupenda kumridhisha kila mtu, kutokupenda kumaliza vitu kwa wakati, uvivu, tamaduni zetu waafrika

kama tulivyoongea hapo juu muda ni nyenzo kuu katika mafanikio yetu hivo tukiutumia vema tutafanikiwa hebu tuangalie ni kwa namna gani tunaweza kuukomboa muda wetuili tuweze kupata mafanikio:-
Panga ratiba yako.
Katika kuutumia vizuri muda ili kupata mafanikio ni lazima tujifunze kupanga ratiba ambayo ndiyo itakayo kuongoza namna ya kuutumia muda, ratiba haiwezi kwenda bila nidhamu, panga ratiba kisha weka nidhamu ya kuifuata ratiba hyo na hakikisha hakuna kikwazo chochote kitakachokufanya uwe nje ya ratiba yako. hapa utaweza kuutawala vizuri muda wako na kupata mafanikio.
Weka vipaumbele.
Mwanadamu hajaumbwa kufanya kila kitu bali ameumbwa kufanya kitu, hivo basi hapa duniani huwezi kufanya kila kitu kwa sababu hauna muda wa kutosha kufanya kila kitu bali unao muda wa kufanya kitu cha muhimu, hivo weka vipaumbele vyako ni vitu gani unafanya kwa muda gani, hivo katika muda husika unaweza kufanya mambo muhimu na yakakuletea mafanikio, hivyo ili kuutawala muda inatupasa tujiwekee vipaumbele, mfano anza kuamka asubuhi na mapema na ipangilie siku yako ni vitu gani unaenda kufanya kwa siku hiyo hivo itakuepusha kupoteza muda.
Epuka kuahirisha mambo (avoid procrastination).
Moja ya sababu kubwa inayopoteza muda ni kuahirisha ahirisha mambo, watu wengi tunapenda kuhairisha mambo kutokana na uvivu na kusema nitafanya kesho, ikifika kesho unasema nitafanya kesho hivo kila siku unasema kesho kesho hivo unajikuta unapoteza muda mwingi kwa sababu ya kuhairisha mambo, hivo epuka kuhairisha hairisha mambo ili kutunza muda, ukipata jambo fanya sasa wazungu wanasema (Do it now) hivo fanya sasa kwa sababu muda si rafiki ukienda haurudi tena.
Jifunze kutenga muda wa ziada.
Mpendwa rafiki sio kila muda ni muda wa kuongea ama kupata burudani ukifanya hivi basi unaukaribisha umaskini kwa mikono miwili, tumia muda wako kufanya mambo yenye tija na mafanikio kwako hivo panga muda wa ziada ambao utautumia kwa ajiri ya kukutana na marafiki, kupata burudani nk

Tumia nafasi zinazopatikana kukamilisha mambo madogo madogo.
Muda ambao unatumia kufanya mambo yako ya msingi zuia mtu yeyote kutaka kuuharibu hivo ukipata muda wa ziada mfano muda wa kula tumia kukamilisha mambo madogo madogo kama kukutana na mtu kwa ajiri ya maongezi ya muda mfupi hapo utakuwa unatumia muda wako vizuri na mafanikio yatakuja tu.
nikutakie siku njema na utumizi mzuri wa muda wako, tumia muda wako vizuri kabla muda haujakutumia wewe.
Mwandishi: fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: 0717262705/0683636572
Email:             fanuelmwasyeba@gmail.com