Karibu mpendwa mfuatiliaji wa mtandao wetu wa Rise Africa, napenda kukukaribisha kwa mala nyingine katika kujadili mambo mbalimbali yahusuyo mafanikio. Nia na lengo kubwa la Rise Africa ni kuona kila kijana wa Africa amefanikiwa.
leo napenda nikushirikishe kuhusu adui wa mafanikio yako. Kila mmoja wetu anamjua vema adui anaemkwamisha kufanikiwa, ata wewe rafiki unamjua fika au unajua vizuri kabisa ni kwanini haufanikiwi au kwanini mpaka leo upo hapo ulipo, swali langu leo kwako mpendwa rafiki, "kwanini unazidi kumlea adui wa mafanikio yako?".
Adui wako katika mafanikio unamjua vizuri inaweza kuwa ni hofu, woga, uvivu, kukata tamaa, na mengine mengi sasa swali kwanini unazidi kulea adui yako wakati unajua hivo ulivo sasa hupigi hatua yeyote, hufanikiwi, miaka inaenda bado uko vile vile.
maswali yangu kwako-
- Je umependa kuwa hapo ulipo mpaka leo?
- Je ni kwanini unaendelea kumlea adui yako?
- Je umeshindwa kujinasua kutoka kwa adui yako?
Kumjua adui yako ni mwanzo wa kujinasua kutoka kwa adui, anza sasa kataa kumlea adui yako chukua hatua sasa badilika, wewe ndie mwenye uwezo wa kubadilika na kumuacha adui anaekwamisha mafanikio yako. soma zaidiHakuna kinachoshindikana kama ukiamua
Tumia nguvu zako zote kukataa kile kinachokukwamisha wewe kufanikiwa, mfano kama adui yako ni hofu kitu cha kufanya cha kwanza jifunze kuikabili hofu,kama unataka kuanzisha biashara na inahitaji mtaji mkubwa na wewe una mtaji mdogo, tumia mtaji huo mdogo kuanzisha biashara ndogoukipata faida endelea kuipanua biashara mpaka kufikia biashara unayoitaka. Soma zaidiUhusiano wa maisha ya tai na mafanikio.