Karibu rafiki katika mtandao wetu wa RISE AFRICA, ni matumaini yangu u mzima wa afya, napenda kukukaribisha tena kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu mafanikio. Katika makala ya leo naomba tujadili kikwazo cha mafanikio ya mtu, watu wengi wanapenda sana kufanikiwa lakini wanajikuta wako pale pale na kuanza kulalamika kwanini hawafanikiwi na kuanza kutupa lawama kwa watu wengine kwamba ndio wamekwamisha mafanikio yao, mimi leo napenda kukuambia kwamba mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe.
Utajiri ni sawa na sumaku ikiwa na maana kubwa katika kuutofautisha umaskini na
Kama ulivyo mvuto wa sumaku kwenye vitu vyenye asili ya chuma, haiba ya utambuzi nayo ni muhimu kwani ni chanzo cha uchumi imara kwa kila mwenye ndoto ya kuwa na mafanikio makubwa.
Utajiri ni sawa na sumaku ikiwa na maana kubwa katika kuutofautisha umaskini na utajiri. Sumaku huvivutia vitu vyenye asili ya chuma na kutofanya chochote kwa visivyo na asili ya chuma kama vile plastiki, mbao au karatasi.
Ili upate mafanikio makubwa unahitaji kuwa na haiba au tabia za utambuzi wa watu waliofanikiwa, au kuendana na tabia zinazovutwa na watu waliofanikiwa. Kutokuwa na maarifa haya kutauchelewesha uhuru wako wa kiuchumi.
Watu walio na mafanikio makubwa maisha yao yana mambo kadhaa ambayo maskini hawana. Kufika huko, hakuna namna zaidi ya kujifunza na kutenda ili kufikia kiwango zaidi ya wachache unaowafahamu.
Ili uwe sumaku ya mafanikio ni muhimu kuwa mwanafunzi wa maisha. Watu wenye mafanikio makubwa kila siku, wao huwa ni wanafunzi wa mafanikio na hutafuta maarifa au taarifa mpya. Maskini walio wengi, wanahisi wanajua kila kitu suala ambalo siyo kweli.
Matajiri wengi wamefanikiwa kwa kujifunza kupitia vitabu vya maendeleo, watu walioendelea, changamoto zao na za wengine. Unaweza kujifunza mengi kupitia maandishi hasa vitabu, majarida, magazeti humo ndimo hujengwa tofauti ya wewe na aliyefanikiwa.
Wengi wetu tunaangamia kwa kukosa maarifa ambayo tunaweza kuyapata kupitia vitabu, magazeti na majarida. Napenda nirudie hapa, wengi wetu ambao hatujafanikiwa huwa hatujishughulishi hata kidogo kujifunza. Nadhani hicho ni sababu iliyokufanya kuwa ulivyo. Anza sasa kuwa mwanafunzi wa maisha yako, isiishie kuwa mwanafunzi wa shule au chuo, kazi yako au mradi wako. Ni muhimu sana, tena kwa zaidi ya asilimia 70 uwe mwanafunzi kuhusu wewe binafsi au utambuzi.
Mtazamo chanya katika maisha ni muhimili muhimu wa kuyafikia malengo makubwa. Mtazamo chanya ni umeme unaonganisha nyaya za akili yako kuwasha nuru ya mafanikio yako. Ukikutana na watu au maneno hasi ni sawa na kutupia maji kwenye tanuri la moto unaowaka.
Soma hii Uhusiano wa maisha ya ndege tai na mafanikio
Watu wengi waliofanikiwa; unaowafahamu na usiowafahamu wako chanya. Chunguza kuanzia sasa, chuki, vinyongo, viko akilini kwa watu maskini. Tajiri hana muda na hizo habari.
Ndiyo maana tajiri yupo karibu na tajiri, maskini na maskini mwenzie au, wakati mwingine peke yake. Matajiri wote wamekuwa wakiwashauri watu wote kuwa chanya na kuepuka mitazamo hasi kwani inapingana na imani ya mafanikio.
Matajiri wote hawalalamiki, ni maskini peke yake anayeilalamikia Serikali, mwalimu, mchungaji, familia, ndugu au marafiki. Mwanasaikolojia wa Marekani, Dk Ben Carson anasema: “Wewe ndiye unayetakiwa kufanya unachokihitaji katika maisha yako.”
Watu wenye mafanikio wanaamini wanayo nafasi ya kubadilisha maisha yao wao wenyewe kuliko mtu mwingine yeyote. Mafanikio uliyonayo leo yanatokana na ulichokifanya wewe mwenyewe, siyo mtu mwingine.
Watu wengi waliofanikiwa hulala kwa saa chache huku muda mwingi wakifanya kazi, au kupanga mikakati ya kuwaongezea kipato ingawa unaweza ukawaona hawashughuliki kwa lolote.
Ni muhumu sasa ukakaa na kamati ya akili yako na kupanga upya muda unaoutumia kulala. Inawezekana ulikuwa hufahamu umuhimu wa kutotumia muda mwingi kitandani, huenda muda ukawa mchawi wako namba mbili.
Soma hii Vitu unavyotakiwa kuviacha kama unataka mafanikio
Hili unaweza ukalithibitisha kwa kuona namna ilivyo vigumu kukutana na watu wengi wenye mafanikio katika jamii. Hata kwako hili linawezekana, ukiona watu wengi wanakukosa na kukuulizia basi ni dalili nzuri ya mafanikio.
Wakati maskini anashinda amelala kitandani kwa kukosa kazi ya kufanya, tajiri huwa hana hata muda wa kulala au kula. Matajiri wote huwa wanafanya kazi muda mrefu. Ukilala utavuna utakachokiota. Malipo ya uvivu hulipa hupatikana leo wakati ya juhudi ni baadaye. Kwa hiyo, acha uvivu fanye kazi.
Ili uwe na mafanikio ni muhimu kuwa na vyanzo zaidi ya kimoja vya mapato. Hapa hakuna mbadala, zaidi ya kuongeza mirija yako inayokuongezea riziki wewe na familia yako.
Ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu alituumba tukiwa na macho mawili, miguu miwili na mikono miwili. Matajiri wamelitambua hili mapema ndiyo maana hakuna tajiri yeyote aliyefanikiwa kwa kuwa na chanzo kimoja cha mapato, tafakari.
Wengi huwa ni wawekezaji katika nyanja mbalimbali za uchumi. Matajiri wengi wanamiliki kampuni kuanzia mbili na kuendelea. Ni maskini pekee anayetegemea chanzo kimoja tu cha mapato, chaweza kuwa mshahara. Mtu ana duka moja, ukimwambia apambane aongeze duka la pili anahisi unamchanganya.
Usijutie kuwapo ulipo, furahia na kuwa na shauku ya kufika mbali ukutakako. Tajiri hajutii kuwa na hali hiyo na siku zote hujivunia utajiri wake. Hata akisemwa kwa lolote baya, hatojuta hata siku moja.
Kuwa maskini au tajiri ni uamuzi ndiyo maana wao huwa hawajutii. Lakini maskini wanajutia kwa masuala mengi waliyopitia, badala ya kurekebisha makosa yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)