FIKRA PEVU: HAKUNA MUDA ZAIDI YA SASA

habari za muda na wakati huu mpendwa rafiki, ni matumaini yangu u mzima wa afya. Nakukaribisha tena katika mtandao wa Rise Africa kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, rafiki kujifunza hakuna kikomo kila siku inabidi ujifunze jambo jipya hapo kutakufanya upige hatua kuelekea mafanikio makubwa.

Watu wengi wanapenda kusema nitafanya kesho au nitafanya baadae, je wewe ni mmoja kati yao?.
Soma zaidi Huu ndio ugonjwa hatari kwa mafanikio yako

Muda ni sehemu kubwa kabisa katika mafanikio yetu, kitu kikubwa ni kwamba muda ukipita haurudi tena katika maisha yako hivo ukiutumia vibaya utazidi kuwa masikini. Tofauti kubwa iliyopo kati ya waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni katika matumizi ya muda, waliofanikiwa wanatumia Muda wanaoupata kutekeleza mambo yanayowaletea mafanikio,  lakini wasiofanikiwa wanapenda kusema "muda bado upo nitafanya baadae au kesho".

Mpendwa rafiki acha nikuambie ukweli tusifarijiane wakati tunazidi kudidimia na kuwa masikini mpaka leo, hebu jiulize mwanzoni mwa mwaka huu uliandika malengo na ukaahidi kuyatekeleza je umeyatekeleza?, ulipanga kuanzisha biashara je umeanzisha?. Hebu kuwa hakimu na mwamuzi wa maisha yako tazama kiundani hivi umebadilika au unazidi kujifariji tu kuwa "aliyekupa wewe ndiye kaninyima mimi".

Tatizo ulilonalo ni kusema nitafanya baadae au kesho, hilo ndilo tatizo kubwa lililokufanya mpaka leo uwe hapo ulipo, unapenda kuhairisha mambo (procrastination) hivo kila siku unasema nitafanya kesho nitafanya kesho mpaka mwaka unaisha unabaki vile vile unapiga hatua kurudi nyuma.

Mpendwa Rafiki muda wa kufanya kazi ni sasa weka juhudi zaidi katika siku yako ya leo panga mambo yako vizuri na tekeleza kwa wakati uliopo, usisubiri kesho wala baadae muda wako ni sasa hakuna muda mwingine wa kutekeleza majukumu yako. Soma zaidi Vitu unavyopaswa kuviacha kama unataka kufanikiwa

Tumia muda wako vizuri kwa kuwa utakapouchezea muda utakuja kujutia, kama sheria ya sababu na matokeo(law of cause and effect), chochote ukifanyacho tarajia matokeo yake, wewe ndiye muamuzi mkubwa wa maisha yako ukitaka mabadiliko amua leo fanya kazi jibidiishe leo usiingoje kesho maana kesho huijui.nikutakie siku njema na jitihada njema za kuhakikisha unafanikiwa.
Mwandishi: Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano: +255717262705/+255683636572
Email.            :fanuelmwasyeba@gmail.com