KILA MTU ANAPENDA KILICHO BORA

. Habari ya asubuhi mpendwa rafiki, natumaini umeamka vema na kuendelea na shughuri za kila siku. Kabla sijaenda kwenye makala ya leo napenda kutoa shukrani kwa wote waliojiunga na ukurasa huu ili tujifunze kwa pamoja ili kufikia malengo yetu, pia tunawakaribisha na wengine kuja kujifunza pamoja nasi. sasa acha twende kwenye makala ya leo KILA MTU ANAPENDA KILICHO BORA, rafiki huitaji shahada kujua unapenda nini katika maisha haya, hii ni sawa na kuuliza kama siku ina mchana na usiku. kiukweli hakuna mtu anayejua kitu gani unapenda zaidi ya wewe mwenyewe, kwa mfano ni wewew ndiye unayeamua leo ule chakula gani bila kupingwa, pia unaweza itumia siku yako kusoma au kwenda kwenye starehe, yaani ni wewe ndiye mwenye kujua nini upendacho. sasa pima hicho ukipendacho kina kuletea faida au hasara kama hasara ni kubwa achana na jambo hilo na badili mwelekeo. ila hulazimishwi kubadilika kwa kuwa mwenye maamuzi ni wewe kwa hyo chukua hatua. Nikutakie siku njema
Mwandishi; Fanuel Mwasyeba
Mawasiliano; 0717262705
Email; fanuelmwasyeba@gmail.com
First