FIKRA PEVU: KAMA UNATAKA MAFANIKIO JIULIZE MASWALI HAYA

Habari za wakati na muda Kama huu mpendwa mfuatiliaji wa mtandao wa Rise Africa ni matumaini yangu u mzima wa afya,karibu tena tukutane kujadili mambo mengi yahusuyo mafanikio, leo ni tarehe moja ya mwezi wa tisa unaweza kufanya mabadiliko na ukafanya makubwa katika maisha na kufanikiwa. Watu wengi wanajiuliza hivi waanzaje kuchukua hatua kufikia mafanikio,wengi wana nia kubwa sana ya kufanikiwa ila hawajui kitu gani kitawasukuma ili kufanya mambo makubwa na kufikia mafanikio makubwa,sasa leo tutaenda kujifunza maswali ya kujiuliza ili kufanya jambo fulani ili kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako.soma zaidiHakuna kinachoshindikana Kama ukiamua

Mafanikio yanahitaji nguvu ya hamasa itakayokusukuma kufanya mambo mbalimbali yatakayokuletea mafanikio, kila siku tunasema hakuna mtu atakayekuletea mafanikio zaidi yako,wewe ndiye utakayeleta mabadiliko katika maisha yako, leo ni tarehe moja mwanzo kabisa mwa mwezi hebu jiambie katika nafsi yako kwamba "leo ni leo sitasubiri kesho,uwanja wangu ni huu na nafasi yangu ya kufanya jambo kubwa ni leo", neno hili litaenda kuleta mabadiliko na nguvu kubwa ya hamasa ya kufanya kila jambo la mafanikio. Soma zaidi Sheria 2: imani (belief).

Sasa twende tutazame maswali ambayo unapaswa kujiuliza Kama unahitaji kufanya jambo lolote na kufikia mafanikio maybes, maswali haya yataanzisha Safari yako ya mafanikio hivo kabla ya kufanya jambo lolote jiulize kwanza maswali haha.
*Nini hasa utambulisho wangu katika Jamie?.
*Je ni lipi lengo langu no mwelekeo wangu?.
*Je ni watu gani napaswa kuambatana nao?.
*Je ni changamoto zipi ambazo navutiwa kuzitatua?.
*Jinsi gani naweza kujenga mtazamo chanya juu ya kile ninachofanya/ninachoenda Logan's?.
*Je nimejiandaa vipi kwenye vikwazo vilivyopo mbele yangu?.
*Je nini furaha yangu?.

Naamini umeelewa na utaenda kutendea kazi,malengo yangu na furaha yangu ni kukuona unapiga hatua kuelekea kwenye mafanikio kuliko kusoma tu na ukaacha bila kuchukua hatua. Anza sasa bado una nafasi ya kubadilisha maisha y'all. Nikutakie siku njema na uende kuchukua hatua sasa.

1 comments:

Ahsante Sana kwa somo hili la leo