Hivi unajua ni kwanini unafanya kazi kwa bidii?, ni sababu ipi iliyo nyuma ya kila kitu unachokifanya?.
Sababu ya vyote hivo tunaiita kusudi lako
Kusudi ni kitu kikubwa kinacholeta maana kubwa na malengo katika maisha yako. Una sababu za msingi za kufanya hicho unachokifanya au huna sababu za hicho unachokifanya, lakini kuwa na uwezo wa kujua "kwanini"ni jambo moja muhimu Sana unalolifanya kwa maisha yako binafsi.
Kama tukiwatazama watu wote wenye ushawishi mkubwa hapa duniani katika historia zao na kujifunza kutoka kwao, inaweza kukurahisishia kutambua kusudi lako hapa duniani.
Kwa mfano, Oprah Winfrey's kusudi lake lilikuwa ni "kuwa mwalimu na kujulikana kwa kuwahamasisha wanafunzi wake kuwa zaidi ya wanavyojifikiria walivyo". Kusudi hili limempelekea kuwa mtangazaji mkubwa anaewasaidia mamilioni ya watu kupitia utangazaji wake na anawaelimisha watu wengi duniani kupitia vipindi vyake vya television.
Mama Teresa kusudi lake lilikuwa ni "kuwafariji wafiwa" hii ilimpelekea katika maisha yake kuwasaidia watu wengi kwa njia mbalimbali, na hili likampelekea kuwa mboni ya kanisa katoliki
Sasa umeshajua kusudi lako?
Kila mtu amekuja duniani kwa kusudi maalumu kuleta mabadiliko hapa dynamo, kitu unachopaswa uanze kufikiria ni kusudi lako ndio chemchem kubwa ya mafanikio yako.
Kusudi lako linakuja kutoka ndani yako, ni kitu kinachosema ndani y'all, kuisikia sauti hii lazima ujiulize maswali haya:-
- Kitu gani ninachokipenda zaidi kukifanya katika maisha yangu?.
- Kitu gani kinaendesha hisia zangu?
Hivo,unahitaji kuwa na kusudi lako unaloenda kulitengeneza, hata Kama sio kubwa, lakini linaweza kutekelezeka na kukamilika. Twende tuangalie hatua 3 za kuandika kusudi lako
- Lengo langu ni (hapa andika nini unataka kufanya na unaenda kufanya kitu hicho kwa Nani).
- Nafanikisha kusudi langu kwa(hapa andika shughuli/kazi unayoenda kuifanya).
- Nitajua Kama nimefanikisha kusudi langu pindi(hapa andika kipimo utakachotumia kutazama Kama umefanikisha kusudi lako).
"Kusudi langu ni kusaidia watu kufanikisha malengo yao haraka zaidi ya ambavyo msaada wangu usingekuwepo, nitafanikisha kwa kufundisha mbinu mbalimbali za mafanikio zitakazo wafanya watu kufanikiwa zaidi ya awali, na nitapima mafanikio ya kusudi langu kwa kuwasaidia zaidi ya watu 10000 kila mwaka na kuona wanapiga hatua kila siku"
Mpendwa rafiki hichi ndicho nilichokuandalia kwa siku ya leo, endelea kuwa nami katika kujifunza zaidi kuhusu mafanikio.
YOUR CHOICE, YOUR LIFE